MAGUFULI ASISITIZA UANZISHWAJI WA MAHAKAMA MAALUM YA MAFISADI AKIINGIA MADARAKANI


 Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama cha Mapinduzi,Dkt John Pombe Magufuli akihutubia maelfu ya wananchi katika viwanja vya Nzovwe mjini Mbeya jioni ya leo,kwenye mkutano wa kampeni ya kuwaomba ridhaa Watanzania ya kuwaongoza katika awamu ya tano.

Dkt Magufuli amesema kuwa serikali atakayoingoza atakapopata ridhaa ya kuingia Ikulu,itazifanya huduma za Afya kuwa bora na kuwabana wahudumu wa afya wenye tabia ya kuchukua dawa na kuziuza kwa watu binafsi.

Magufuli ambaye yupo katika mikoa ya Nyanda za juu kusini katika kampeni ya kusaka nafasi ya kuwa raisi wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania,amesema suala la afya litakuwa moja ya ajenda zake muhimu atakapoingia madarakani.

Katika hatua nyingine Dkt Magufuli amewaleza wananchi kuwa iwapo watampa ridhaa ya kuiongoza Tanzania,atahakikisha anaanzisha mahakama maalumu ya Mafisadi na Wala rushwa.

PICHA NA MICHUZI JR-MBEYA.
 Mbunge wa zamani wa jimbo la Kyela Mzee John Mwakipesile akimpigia debe Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania kupitia Chama cha Mapinduzi CCM Dkt  John Pombe Magufuli wakati mgombea huyo alipofika jimboni humo kuomba kura za wananchi ili wamchague kuwa rais.Mzee Mwakipesile amesema kuwa anamuunga mkono Dkt Magufuli na atahakikisha anashiriki kikamilifu kuhakikisha mgombea huyo anaibuka na ushindi kwa kishindo.
Mgombea Ubunge wa Jimbo la Kyela Dkt Harrison Mwakyembe akimpigia debe Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania kupitia Chama cha Mapinduzi CCM Dr. John Pombe Magufuli wakati wa mkutano wa kampeni uliofanyika katika viwanja vya Nzovwe mjini
 Wananchi wakishangilia jambo kwenye mkutano wa kampeni 
 Mh.David Mwakyusa akimwombea kura mgombea Urais wa CCM Dkt Magufuli kwa wananchi ili apate ridhaa ya kuwatumikia wananchi akiwa Ikulu.
 Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli akiwahutubia wananchi wa Tukuyu mjini kwenye kutano wa kampeni uliofanyika katika uwanja wa Tandale mjini gumo jioni ya leo.

Post a Comment

Previous Post Next Post