Mgombea
Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama cha Mapinduzi,Dkt
John Pombe Magufuli akihutubia maelfu ya wananchi katika viwanja vya
Nzovwe mjini Mbeya jioni ya leo,kwenye mkutano wa kampeni ya kuwaomba
ridhaa Watanzania ya kuwaongoza katika awamu ya tano.
Dkt
Magufuli amesema kuwa serikali atakayoingoza atakapopata ridhaa ya
kuingia Ikulu,itazifanya huduma za Afya kuwa bora na kuwabana wahudumu
wa afya wenye tabia ya kuchukua dawa na kuziuza kwa watu binafsi.
Magufuli
ambaye yupo katika mikoa ya Nyanda za juu kusini katika kampeni ya
kusaka nafasi ya kuwa raisi wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania,amesema
suala la afya litakuwa moja ya ajenda zake muhimu atakapoingia
madarakani.
Katika
hatua nyingine Dkt Magufuli amewaleza wananchi kuwa iwapo watampa ridhaa
ya kuiongoza Tanzania,atahakikisha anaanzisha mahakama maalumu ya
Mafisadi na Wala rushwa.
PICHA NA MICHUZI JR-MBEYA.
Mbunge
wa zamani wa jimbo la Kyela Mzee John Mwakipesile akimpigia debe
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania kupitia Chama cha
Mapinduzi CCM Dkt John Pombe Magufuli wakati mgombea huyo alipofika
jimboni humo kuomba kura za wananchi ili wamchague kuwa rais.Mzee
Mwakipesile amesema kuwa anamuunga mkono Dkt Magufuli na atahakikisha
anashiriki kikamilifu kuhakikisha mgombea huyo anaibuka na ushindi kwa
kishindo.
Mgombea
Ubunge wa Jimbo la Kyela Dkt Harrison Mwakyembe akimpigia debe Mgombea
Urais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania kupitia Chama cha Mapinduzi CCM
Dr. John Pombe Magufuli wakati wa mkutano wa kampeni uliofanyika katika
viwanja vya Nzovwe mjini
Wananchi wakishangilia jambo kwenye mkutano wa kampeni
Mh.David
Mwakyusa akimwombea kura mgombea Urais wa CCM Dkt Magufuli kwa wananchi
ili apate ridhaa ya kuwatumikia wananchi akiwa Ikulu.
Mgombea
Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli akiwahutubia wananchi wa Tukuyu
mjini kwenye kutano wa kampeni uliofanyika katika uwanja wa Tandale
mjini gumo jioni ya leo.
إرسال تعليق