James Mbatia ni mmoja wa Viongozi wa Umoja wa UKAWA, ambaye jana alikutana na Waandishi wa Habari kwenye Ofisi za Makao Makuu ya NCCR- Mageuzi, Ilala Dar
Miongoni
mwa mambo aliyoyazungumzia ni UKAWA kuzuiwa kutumia Uwanja wa Taifa
kwenye uzinduzi wa Kampeni zao, na kutoonekana kwa Dk. Slaa .
“Kampeni
zinaanza nawasihi Wanasiasa wote wachunge ndimi zao sana, tujadili hoja
kwa hoja kwenye majukwaa ya kisiasa sio kujadili watu, matusi, wala
kupigana ngumi au kumwaga damu…
"Tume
ya Uchaguzi ambayo ndio refa itende haki pamoja na vyombo vya dola…
Wakitenda haki hakuna mgogoro wa aina yoyote, Kamati za Ulinzi na
Usalama Wakuu wa Mikoa na Wakuu wa Wilaya hatutaki waingilie mchakato
huu.“ alisema Mbatia
Kuhusu kuzuiwa Uwanja wa Taifa Dar, Mbatia alisema; “Uwanja
wa Taifa ni mali ya Watanzania, tutakutana tutatafakari alafu
tukishakubaliana kwa pamoja tutatoa taarifa wapi tutakutana na
tutazungumza nini, kwa kweli hatuna majibu mpaka sasa hivi,"
Kuhusu swala la Dk. Slaa kutoonekana kwenye Vikao vya UKAWA, Mbatia alisema;
“UKAWA
sio Mbatia, sio Slaa sio Lipumba sio Mbowe… tusijadili watu tujadili
hoja za msingi za taifa, watu wanapita, tuzungumzie Watanzania zaidi“
إرسال تعليق