Klabu
ya Manchester United imekuwa miongoni mwa klabu ambazo zimetambulisha
jei zao leo zitakazotumiwa kwa ajili ya msimu ujao. Klabu hiyo imevunja
rekodi kwa kuwa ni klabu inayoingiza kipato kikubwa cha pesa duniani
kutokana na utengezaji wa jezi .
Baada
ya miaka 13 ya matumizi ya jezi za Nike, Manchester United sasa imeamua
kuzindua jezi mpya zitakazotumika katika msimu wa 2015/2016. Man United
watatumia jezi zitakazokuwa zinatengenezwa na Kampuni ya vifaa vya
michezo ya Adidas ya nchini Ujerumani.
Man
United wamesaini mkataba wa miaka 10 na kampuni ya hiyo ya Adidas,
mkataba wenye thamani ya pound milioni 750 na sasa wataanza kutumia jezi
za kampuni hiyo.
Wakongwe
hao (Adidas) wa kutengeneza vifaa vya michezo wanaamini wanaweza
kutengeneza kiasi cha pauni bilioni 1.5 kutokana na mauzo ya jezi za Man
U kwa muda wa miaka 10 ijayo.
Mkataba
huo kati ya Manchester United na Adidas ni mkataba mnono zaidi kwa
klabu hiyo ukilinganisha mikataba ya klabu nyingine ambazo
zinatengenezewa jezi na kampuni hiyo ikiwa ni pamoja na klabu Bayern
Munich (pauni milioni 645) na Chelsea (pauni milioni 300).
Jezi hizo mpya zitakuwa na muonekano
kama ule wa zamani enzi za Ryan Giggs zikiwa na shingo ya V yenye rangi
nyeupe na michirizi mitatu kwenye mikono yake.
إرسال تعليق