Mshindi wa TMT 2015 #mpakakieleweke apokelewa kwa nderemo mjini Moshi


Baadhi ya ndugu, jamaa na marafiki wa Mshindi wa Shindano la TMT 2015 #mpakakieleweke Dennis Lwasai wakiwa na bango linalomwelezea mahindi huyo wakati walipojitokeza kumpokea wakati akirejea nyumbani kwao Mambogini Moshi.(Picha zote na Josephat Lukaza wa Lukaza Blog).
Mshindi wa TMT 2015 #mpakakieleweke Dennis Lwasai akiwasalimia wakazi wa mji wa Moshi waliokuwa wakimpongeza wakati akirejea kwao Mambo.
Wakiendelea kumpongeza.
Wakitoa Mkono wa pongezi kwa mshindi wakati akipita kuelekea nyumbani kwao.
Akipongezwa na wadau wake.
Kwa hisia huku akifurahi.
Alipokelewa hivi na vijana wenzie.
 Kila Kona walijitokeza wadau kumpongeza
Ndugu, Jamaa na marafiki wakimpokea mshindi wao na kumpongeza kwa kuibuka mshindi na kuiwakilisha kanda ya kaskazini vyema
Mama Mzazi wa Mshindi wa TMT 2015, Dennis Lwasai akimkumbatia mwanae na kumpongeza kwa kuibuka kinara wa TMT 2015 na kuondoka na kitita cha Shilingi Milioni 50 za kitanzania
Mama mzazi wa mshindi wa TMT 2015, Dennis Lwasai akitoa maneno ya shukrani kwa vijana na watu waliojitokeza kumpokea Dennis wakati akirejea kwao Moshi hapo jana.
Dennis Lwasai mshindi wa shindano la TMT 2015 #mpakakieleweke akitoa maneno ya shukrani kwa vijana na watu wote waliojitokeza kumpokea mapema jana wakati akirejea nyumbani Kwao Moshi

Post a Comment

Previous Post Next Post