News:- Taarifa kwa Vyombo vya Habari Zanzibar.4.8.2015.

Kwa mujibu wa uwezo aliopewa chini ya kifungu namba 48 na kifungu 129 vya Katiba ya Zanzibar, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohammed Shein amekubali ombi la kujiuzulu kwa Mhe. Juma Duni Haji, aliyekuwa Waziri wa Miundombinu na Mawasiliano Zanzibar. kujiuzulu kuaza tarehe 01 Agosti, 2015.
Taarifa hii imetiwa saini na Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Ikulu Ndg Salum M. Salum,kwa niaba ya Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi Zanzibar.
Leo 04 Agosti, 2015.

IMETOLEWA NA HABARI MAELEZO ZANZIBAR.

Post a Comment

Previous Post Next Post