Wachezaji wa timu ya Simba wakipongezana baada ya kuwafunga Jang'ombe Boys
Mfungaji wa moja ya magoli ya Suimba Elia maguri akidhibitiwa vilivyo na beki wa Jang'ombe Boys
Na Ameir Khalid
ELIAS
Maguri ameendelea kutesa kwa kuzifumania nyavu kisiwani Zanzibar,
ambako klabu yake Simba SC imekuwa kambini ikicheza mechi za kujipima
nguvu.
Jioni
hii, Maguri alifunga bao moja wekundu hao wakishinda 3-0 dhidi ya
Jang’ombe Boys iliyopanda Ligi Kuu msimu ujao, katika uwanja wa Amaan.
Simba
inayofundishwa na kocha Muingereza Dylon Kerr anayesaidiwa na mzalendo
Selemani Matola, ilianza kuzihujumu nyavu za wapinzani wao katika dakika
ya 14, Maguri akiwa ndiye mfungaji.
Dakika
ya 17, Jang’ombe Boys wakamruhusu Michael Mgimwa kuandika bao la pili,
na timu hizo zikaenda mapumziko Simba ikiongoza 2-0.
Simba ilihitimisha ushindi wao kwa bao la dakika ya 81 lililopachikwa kimiani na Samir Omar.
Huo
ni mchezo wa nne kwa Simba SC kucheza na kushinda tangu ilipanza kambi
yake kisiwani hapa mwanzoni mwa wiki iliyopita, awali ikiifunga kombaini
ya Zanzibar 2-1, ikaitandika Black Sailors 4-0, Polisi 2-0 kabla
leo kupata ushindi huo wa 3-0 dhidi ya Jang’ombe Boys.
Simba
itakamilisha mechi zake Jumatano kwa kupambana na KMKM iliyotolewa
hatua za makundi kwenye michuano ya kombe la Kagame iliyomalizika
Jumapili, kabla ya kurejea Dar es Salaam Alkhamisi.
إرسال تعليق