Waziri wa Uchukuzi, Samwel Sitta, akizungumza na wanahabari (hawapo pichani).
Sitta akisisitiza jambo.
Wanahabari wakichukua matukio katika hafla hiyo.
Wanahabari wakifuatilia tukio.
WAZIRI wa
Uchukuzi, Samwel Sitta, amemjibu Waziri Mkuu mstaafu, Frederick Sumaye,
baada ya kuituhumu serikali ya Rais Kikwete kuwa imewafumbia macho
watendaji walioisababishia hasara nchi zaidi shilingi bilioni 220 kwenye
ununuzi wa mabehewa yanayotajwa kuwa ni feki.
Akizungumza na wanahabari kwenye ofisi za wizara yake, Sitta amesema
watendaji wote waliohusika na kashfa hizo watafikishwa mahakamani muda
wowote kutoka sasa baada uchunguzi kukamilika.
Aliongeza kwamba kamati iliyoundwa kuchunguza sakata hilo
imeshakamilisha kazi yake na kuonesha kulikuwa na uzembe kwa watendaji
wa shirika la reli (TRL) uliosababisha kununuliwa kwa mabehewa hayo.
Aidha amesema kuwa kamati hiyo ilikwenda hadi nchini India kuichunguza kampuni ya M/S Hindusthan Engineering and Industrial Limited ambayo ndiyo watengenezaji wa mabehewa hayo mabovu na kubaini kampuni hiyo iliyopewa zabuni ilikuwa haina sifa.
Aidha amesema kuwa kamati hiyo ilikwenda hadi nchini India kuichunguza kampuni ya M/S Hindusthan Engineering and Industrial Limited ambayo ndiyo watengenezaji wa mabehewa hayo mabovu na kubaini kampuni hiyo iliyopewa zabuni ilikuwa haina sifa.
Hata hivyo, Sitta ameongeza kuwa kamati hiyo ilibaini kampuni hiyo
haikuwa na sifa na watendaji TRL walikiuka kanuni za manunizi ya
serikali kwa kitendo chao cha kutoa fedha zote kwa kampuni hiyo kabla
hawajaleta mabehewa.
Viongozi wanaotuhumiwa katika sakata hilo kuwa ni Mkurugenzi Mtendaji wa
TRL, Kipallo Kisamfu; Mhandisi Mkuu wa Mitambo, Ngosowile Ngosomiles;
Mhasibu Mkuu Mbaraka Mchopa; Mkaguzi Mkuu wa Ndani wa Kampuni, Jasper
Kisiraga; na Meneja Mkuu wa Manunuzi, Ferdinand Soka.
(NA DENIS MTIAMA/GPL)
إرسال تعليق