OFISI
ya Makamu wa Rais inasikitika kuwepo kwa taarifa ambazo zimesambaaa
kwenye mitandao ya kijamii zinazodai kuwa Mheshimiwa Makamu wa Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal ataongea na
vyombo vya habari kuhusu msimamo wake ndani ya serikali na Chama Cha
Mapinduzi.
Tunaomba kuueleza umma wa Watanzania kuwa Mheshimiwa Makamu wa Rais
hajapanga tukio lo lote la kukutana na waandishi wa habari na wala hana
mpango wa kuzungumzia msimamo wake ndani ya Serikali na Chama Cha
Mapinduzi.
Tunatumia
nafasi hii kuwataka wale wote wenye tabia ya kuvumisha taarifa zisizo
sahihi waache kufanya hivyo kwa kuwa ni kosa kisheria. Tunawaomba
waandishi wa habari kufuata taratibu za kazi na kutafuta taarifa sahihi
kwenye vyombo vinavyotambulika.
Boniphace Makene
Mwandishi wa Habari wa Makamu wa Rais.
إرسال تعليق