Chama
cha wafanyakazi madereva Tanzania-TADWU- kimetangaza mgomo wa madereva
nchi nzima kuanzia Agosti tisa mwaka huu baada ya wamiliki wa mabasi,
wakala wa usafiri wa nchi kavu na majini pamoja na wizara ya kazi
kushindwa kutekeleza makubaliano yalifikiwa na tume iliyoundwa na waziri
mkuu kutatua mgogoro wa madereva nchni.
Kauli hiyo imetolewa na naibu katibu mkuu wa TADWU, Bwana Rashidi
Salehe wakati akizungumza na ITV ambapo amesema mgomo huo unarejea tena
baada ya wamiliki wa mabasi kwa kushirikiana na wizara kazi pamoja na
Sumatra kuendelea kutumia mikataba ya zamani katika kutoa leseni wakati
makubaliano ya tume iliyoundwa na waziri mkuu yalitaka mikataba mipya
ianze kutumika kuanzia julai mosi mwaka huu.
Wakizungumza na ITV baadhi ya madereva wamelalamikia wizara ya kazi
na sumatra kwa kukaidi agizo la waziri mkuu na kuendelea kupokea
mikataba ya zamani toka kwa wamiliki wa mabasi na kutoa leseni wakati
makubaliano yalishafanyika na kusisitiza katika makubaliano hayo
mishahara ya madereva wa malori yanayotoka nje ya nchi walikuwa
wanatakiwa kulipwa mishahara ya shilingi milioni moja, huku madereva wa
daladala shilingi laki tano pamoja na posho nyingine.
Akizungumza kwa simu na mmoja wa viongozi wa chama cha wamiliki wa
mabasi nchni kwa masharti ya kutotajwa jina amewalalamikia madereva hao
kwa kupanga mgomo badala ya kupeleka madai yao kwa tume ya kudumu
iliyoundwa na waziri mkuu ili kupata ufumbuzi ambapo amesema kuna baadhi
ya madereva wanatengeneza migomo ili kuleta usumbufu kwa wananchi na
serikali kwa ujumla.
إرسال تعليق