Mkurugenzi
Mkuu wa Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA), Hiiti Sillo (kushoto),
akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Makao Makuu ya TFDA
Dar es Salaam leo, wakati akitoa tahadhari ya uwepo katika soko wa
vipodozi vyenye viambato vilivyopigwa marufuku na Serikali. Kulia ni
Mkurugenzi wa Dawa na Bidhaa Nyongeza, Fimbo Mitungu.
Mkurugenzi
wa Dawa na Bidhaa Nyongeza, Fimbo Mitungu (kushoto), akizungumza
katika mkutano huo huku akionesha moja ya kopo lenye kipodozi
vilivyopigwa marufuku. Kulia ni Kaimu Mkurugenzi Uendelezaji Hudumawa TFDA, Chrispin Severe
Baadhi ya vipodozi hivyo ambavyo vina madhara kwa matumizi ya binadamu |
Mamlaka ya chakula na
dawa nchini Tanzania TFDA leo wametangaza uwepo wa aina ya vipodozi aina 36
ambazo ni feki na ni hatari kwa matumizi ya binadamu na kuwataka wananchi kuwa
makini katika kununua aina hiyo.
Akizungumza na
wanahabari leo Jijini Dar es salaam mkurugenzi wa TFDA Hiiti Sillo amesema kuwa
wanautaarifu umma kuwa kupitia mfumo wake wa ufwatiliaji ubora na usalama wa
bidhaa kwenye soko imebaini uwepo wa vipodozi vyenye viambato vilivyopigwa
marufuku aina ya STEROIDS zinazojulikana kitaalam kama CLOBETASOL
PROPIONATE,HYDROCORTISONE na TRIAMCINOLONE.
Amesema kuwa aina ya
vipodozi tofauti 36 vya jamii ya krimu na losheni vimebainika kuwa na viambato
hivyo vilivyopigwa marufuku baada ya kufanya uchunguzi wa kina wa matoleo 57
yaliyochukuliwa kwenye soko na viwanda vinavyotengeneza.
Vipodozi hivyo
vimetengenezwa na makampuni manne yaliyopo nchini Tanzania na kampuni moja
kutoka nchini Africa kusini.makampuni hayo ni
–CHEMI-COTEX INDUSTRIES
LIMITED-DAR ES SALAAM
-MAMUJEE PRODUCT
LIMITED-TANGA
-TANGA PHARMACEUTICAL
AND PLASTICS LIMITED-TANGA
-TRIDEA COSMETICS
LIMITED-DAR ES SALAAM
-JOHNSON AND JOHNSON
LIMITED –AFRICA KUSINI.
Amesema kuwa baadhi ya
madhara makubwa yatikanayo na vipodozi hivyo ni pamoja na kuvimba
mwili,muwasho,ngozi kiwaka moto,ngozi kukatika katika,ngozi kubabuka,kuwa nyeupe
isiyokuwa ya kawaida,madhara kwenye mifupa,kizunguzungu,pamoja na madhara
mengine mengi ikiwemo kiznguzungu na kichwa kuuma.
Baada ya kugundua dawa
hizo kuwepo sokoni TFDA imezuia kwa muda wa mkiezi sita utengenezaji wa
vipodozi aina ya krimu,losheni,na jeli kwenye viwanda vinne ambavyo vimekutwa
na makosa hayo.
Wenye viwanda hivyo
wameelekezwa kuviondoa vipodozi hivyo sokoni na kuviteketeza kwa gharama yao.
TFDA imefuta usajili wa
vipodozi 31 vilivyokuwa vimesajiliwa.
Pia ukaguzi zaidi
kutoka kwa mameneja wa TFDA ili kubaini aina nyingine ya bidhaa zilizopo sokoni
ambazo sio nzuri kwa mwanadamu.
Post a Comment