Eti Lulu alilia kuzaa kwa gharama yoyote anatamani mtoto!



MAKUBWA! Akiwa angali na umri wa miaka 20, staa wa sinema za Kibongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’ amenyanyua kinywa chake na kutamka kuwa anataka kuzaa kwa gharama yoyote kwani anatamani sana mtoto.

Kauli hiyo ameitoa Lulu mara baada ya mwanahabari wetu kumuuliza sababu za yeye kupenda kuweka watoto wadogo katika mitandao ya kijamii ndipo Lulu alipofunguka kuwa anatamani sana kupata mtoto.

“Yaani asikwambie mtu, nalilia kweli kupata mtoto japo wengi wanaweza kuona kwamba bado umri wangu  ni mdogo lakini kwangu mimi naona kama umri unaniacha hivi natamani hata huu mwaka usiishe niwe tayari na mimi napakata kichanga changu,” alisema Lulu na kuongeza:

“Kwa kweli hata kama ni kwa gharama yoyote itabidi inigharimu ili na mimi niitwe mama maana furaha yangu ya moyo haiwezi kukamilika kama sijaitwa mama na mimi.”

Lulu aliwahi kuwa mpenzi wa marehemu mwigizaji Steven Kanumba, hawakufanikiwa kupata mtoto achilia mbali wanaume kadhaa kudaiwa kutembea naye lakini bado mambo hayajajipa!

Post a Comment

Previous Post Next Post