MAKUBWA!
Akiwa angali na umri wa miaka 20, staa wa sinema za Kibongo, Elizabeth
Michael ‘Lulu’ amenyanyua kinywa chake na kutamka kuwa anataka kuzaa kwa
gharama yoyote kwani anatamani sana mtoto.
Kauli hiyo ameitoa
Lulu mara baada ya mwanahabari wetu kumuuliza sababu za yeye kupenda
kuweka watoto wadogo katika mitandao ya kijamii ndipo Lulu alipofunguka
kuwa anatamani sana kupata mtoto.
“Yaani asikwambie mtu, nalilia
kweli kupata mtoto japo wengi wanaweza kuona kwamba bado umri wangu ni
mdogo lakini kwangu mimi naona kama umri unaniacha hivi natamani hata
huu mwaka usiishe niwe tayari na mimi napakata kichanga changu,” alisema
Lulu na kuongeza:
“Kwa kweli hata kama ni kwa gharama yoyote
itabidi inigharimu ili na mimi niitwe mama maana furaha yangu ya moyo
haiwezi kukamilika kama sijaitwa mama na mimi.”
Lulu aliwahi kuwa
mpenzi wa marehemu mwigizaji Steven Kanumba, hawakufanikiwa kupata
mtoto achilia mbali wanaume kadhaa kudaiwa kutembea naye lakini bado
mambo hayajajipa!
إرسال تعليق