Mkemia Mkuu wa Serikali kuwachukulia hatua wadau wasiosajiliwa


Profesa Manyele_0
Mkemia Mkuu wa Serikali Prof. Samwel Manyele. (Picha na Maktaba).
Na Beatrice Lyimo, Maelezo
Ofisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali imewataka wadau wote wanaojihusisha na usafirishaji na uuzaji wa kemikali kujisajili kabla ya hatua za kisheria hazijachukuliwa dhidi yao.
Kauli hiyo imetolewa jana jijini Dar es salaam na Mkemia Mkuu wa Serikali Prof. Samwel Manyele wakati wa warsha ya siku moja iliyolenga kuwaelimisha wadau wa uuzaji na usafirishaji kuhusiana na usimamizi wa kemikali hatari na zenye madhara kwa afya na mazingira kwenye maeneo ya bandari na wakati wa usafirishaji.
Amefafanua kuwa Sheria ya Usimamizi na Udhibiti wa Kemikali za Viwandani na Majumbani Na. 3 ya mwaka 2003 inawataka wadau kusajiliwa ili kuhakikisha kuwa kemikali zinatumika katika hali iliyosalama wakati wa kusafirishwa,kuuzwa na kuhifadhi.
 “Katika kuendelea kuimarisha utekelezaji wa Sheria ya Usimamizi na Udhibiti wa Kemikali za Viwandani na Majumbani, Wakala wa Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali umekuwa ukifanya jitihada kadhaa kuhakikisha wadau wote wanauelewa wa kutosha kuhusiana na maswala ya sheria” alisisitiza Prof. Manyele.
Alisema kuwa Ofisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali imekuwa ikijitahidi kutoa elimu kwa wadau kupitia warsha, mikutano, ukaguzi, kushiriki kwenye maonyesho, mafunzo kwa wasimamizi wa shughuli zinazohusiana na masuala ya kemikali na madereva wanaosafirisha kemikali ili kuhakikisha kuwa wadau na wananchi wanatumia kemikali katika hali iliyosalama kwao na mazingira.
Mbali na hayo warsha hiyo imewakutanisha wadau muhimu wa Bandari kwa lengo la kupeana elimu na kujadili juu ya namna bora ya kusimamia upakiaji, upakuaji, na uhifadhi wa shughuli yeyote inayohusu kemikali hatari katika maeneo ya Bandari.
Aidha Mkemia Mkuu huyo wa Serikali alisema kuwa Ofisi hiyo inaanda warsha nyingine ya kuelimisha wadau juu ya kuchukua taadhari juu ya kujikinga na tukio ambalo linaweza kutokea kutokana na mlipuko wa kemikali kama ilivyokea nchini China

Post a Comment

أحدث أقدم