Rais
Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akikata utepe kufungua jengo la kitega
uchumi la Shirika la Nyumba la Taifa(National Housing Corporation) NHC
Lumumba Complex mjini Kigoma leo .Wengine katika picha ni Mke wa Rais
Mama Salma Kikwete,(watatu kushoto), Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo
ya Makazi Mh.William Lukuvi,(wanne kushoto), Mkuu wa mkoa wa Kigoma
Issa Machibya,(Wapili kulia), Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la
Taifa NHC Bwana Nehemia Mchechu(kulia), na kushoto ni Mbunge Mstaafu wa
Jimbo la Kigoma mjini Mh.Peter Selukamba.
Rais
Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akifunua jiwe katika jiwe kuashiria kufungua
rasmi jengo la kitega uchumi la Shirika la Nyumba la Taifa National
Housing Lumumba Business Complex mjini Kigoma leo.Wapili kushoto ni Mke
wa Rais Mama Salma Kikwete na watatu kushoto ni Mkurugenzi mkuu wa NHC
Bwana Nehemia Mchechu.
Jengo la Kitega uchumi Lumumba Business Complex, lililofunguliwa na Rais Kikwete mjini Kigoma leo.
Rais
Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akifunua kitambaa katika jiwe la msingi
wakati wa hafla ya uzinduzi mradi wa nyumba za bei nafuu NHC eneo la
Mlole mjini Kigoma leo.Rais Kikwete yupo mkoani Kigoma kwa ziara ya
kikazi ya siku mbili. Kulia ni Waziri wa Ardhi Nyumba na maendeleio ya
Makazi Mh.William Lukuvi,Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Issa Machibya
na watatu kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa(NHC)
Bwana Nehemia Mchechu,
Rais
Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akikata utepe wakati wa uzinduzi wa nyumba za
bei nafuu zilizojengwa na Shirika la Nyumba la Taifa NHC eneo la Mlole
mjini Kigoma leo. Wengine katika picha ni Waziri wa Ardhi Nyumba na
Maendeleo ya Makazi Mhe.William Lukuvi(wapili kushoto), Mkuu wa Mkoa wa
Kigoma Issa Machibya(wapili kulia), Mbunge mstaafu wa Kigoma mjini
Mh.Peter Selukamba(wanne kjshoto), Mkurugenzi mkuu wa NHC Bwana Nehemia
Mchechu kulia na kushoto ni Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Kigoma Ndugu Walid
Kabouru.
Rais
Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwapungia mamia ya wakazi wa mji wa kigoma
wakati akingia katika uwanja wa michezo wa Lake Tanganyika ambnapo
alihutubia Mkutano wahadhara na kuwaaga rasmi wananchi wa mkoa wa
Kigoma(picha na Freddy Maro)
Post a Comment