Rais Kikwete azindua miradi ya Maendeleo kigoma awaaga wananchi

 


 Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akikata utepe kufungua jengo la kitega uchumi la Shirika la Nyumba la Taifa(National Housing Corporation) NHC Lumumba Complex mjini Kigoma leo .Wengine katika picha ni Mke wa Rais Mama Salma Kikwete,(watatu kushoto), Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mh.William Lukuvi,(wanne kushoto), Mkuu wa mkoa wa Kigoma Issa Machibya,(Wapili kulia), Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa NHC Bwana Nehemia Mchechu(kulia), na kushoto ni Mbunge Mstaafu wa Jimbo la Kigoma mjini Mh.Peter Selukamba.
 Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akifunua jiwe katika jiwe kuashiria kufungua rasmi jengo la kitega uchumi la Shirika la Nyumba la Taifa National Housing Lumumba Business Complex mjini Kigoma leo.Wapili kushoto ni Mke wa Rais Mama Salma Kikwete na watatu kushoto ni Mkurugenzi mkuu wa NHC Bwana Nehemia Mchechu.
Jengo la Kitega uchumi Lumumba Business Complex, lililofunguliwa na Rais Kikwete mjini Kigoma leo.

 Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akifunua kitambaa katika jiwe la msingi wakati wa hafla ya uzinduzi mradi wa nyumba za bei nafuu NHC eneo la Mlole mjini Kigoma leo.Rais Kikwete yupo mkoani Kigoma kwa ziara ya kikazi ya siku mbili. Kulia ni Waziri wa Ardhi Nyumba na  maendeleio ya Makazi Mh.William Lukuvi,Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Issa Machibya na watatu kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa(NHC) Bwana Nehemia Mchechu,
 Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akikata utepe wakati wa uzinduzi wa nyumba za bei nafuu zilizojengwa na Shirika la Nyumba la Taifa NHC eneo la Mlole mjini Kigoma leo. Wengine katika picha ni Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe.William Lukuvi(wapili kushoto), Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Issa Machibya(wapili kulia), Mbunge mstaafu wa Kigoma mjini Mh.Peter Selukamba(wanne kjshoto), Mkurugenzi mkuu wa NHC Bwana Nehemia Mchechu kulia na kushoto ni Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Kigoma Ndugu Walid Kabouru.
 Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwapungia mamia ya wakazi wa mji wa kigoma wakati akingia katika uwanja wa michezo wa Lake Tanganyika ambnapo alihutubia Mkutano wahadhara na kuwaaga rasmi wananchi wa mkoa wa Kigoma(picha na Freddy Maro)

Post a Comment

أحدث أقدم