Mgombea
 wa Urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akihutubia wakazi wa 
Ifakara wilayani Kilombero kwenye mkutano wa kampeni za CCM ambapo 
aliwaambia wananchi hao kuwa wakati wake utakuwa wa kiutendaji zaidi ili
 kufanikisha maendeleo ya haraka kwa nchi na wananchi kwa jumla.
PICHA NA MICHUZI JR-KILOMBERO.
  
Wananchi wa mji wa Ifakara waliojitokeza kwa wingi kwenye mkutano wa 
kampeni za CCM ndani ya uwanja wa saba saba wilayani 
Kilombero,wakimshangilia kwa shangwe Mgombea Urais wa CCM Dkt Magufuli 
alipowahutubia kwenye mkutano huo.
  Mgombea
 wa Urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akimtambulisha mgombea 
ubunge jimbo la ilombero Ndugu Abubakar Assenga almaarufu kama mtoto wa 
fundi Cherehani kwenye mkutano wa kampeni za CCM zilizofanyika Ifakara 
wilayani Kilombero.
 Mgombea wa Urais kupitia CCM Dk. John Pombe
Magufuli akihutubia wakazi wa Ifakara wilayani Kilombero kwenye mkutano wa
kampeni za CCM ambapo aliwaambia wananchi hao kuwa wakati wake utakuwa wa
kiutendaji zaidi ili kufanikisha maendeleo ya haraka kwa nchi na wananchi kwa
jumla.
MGOMBEA
urais
 kwa tiketi ya CCM, Dk.John Magufuli amesema iwapo atachaguliwa katika
uchaguzi mkuu mwaka huu na kufanikiwa kuunda Serikali yake atahakikisha 
baadhi
ya mambo ya msingi atayaamua kwa kupata ushauri wa marais 
waliomtangulia,amesema kuwa katika kipindi hiki cha kuomba ridhaa ya 
wananchi ili awe Rais hatakuwa
tayari kutoa matumani hewa ambayo anajua wazi hayatekelezeki kwani ni 
dhambi na
kufafafanua kila anachoahidi anauhakika anao uwezo wa kutekeleza.
Akizungumza
kwenye mikutano yake mbalimbali ya kuomba ridhaa ya kuwania urais, Dk.Magufuli
aliwambia wananchi wa Ulanga kuwa anatambua dhamana anayoomba kwa wananchi lakini
ana uhakika malengo yake ya kuwatumikia Watanzania na kuleta maendeleo
yatafanikiwa kwani iwapo atahitaji ushaauri ataupata kwa viongozi
waliomtangulia kuongoza nchi.
Alisema
sifa kubwa ya Tanzania ni kwamba kuna viongozi wastaafu wengi wakimo marais
ambao wametanguli kuongoza nchi kuanzia awamu ya pili, ya tatu na awamu ya nne.
“Iwapo
nahitaji ushauri, wapo viongozi wengi wa kunisaidia kuniongoza .Yupo mzee Ali
Hassan Mwinyi(Rais awamu ya pili), Rais mstaafu Benjamin Mkapa, Rais Jakaya
Kikwete,Rais mstaafu Salimn Amour na Rais mstaafu Aman Abeid Karume.
“Huu
ndio utaratibu wan chi yetu kwamba wapo viongozi wa kutosha wa kunipa ushauri
katika kutekeleza majukumu yangu ya kuwatumikia Watanzania.Najua msimamo wangu
na Serikali nitakayoiunda ni kufanya kazi tu.Narudia tena kwangu mimi ni kazi
tu lakini bado ninao wazee wa kunishauri ili nifikie malengo yangu,”alisema.
Alisema
kiongozi mzuri ni Yule ambaye anaweka malengo ya kuwatumikia wananchi kwa
misingi ya uzalendo na uadilifu na anapoona kuna mambo yanahitaji ushauri kabla
ya kufikia uamuzi wapo viongozi wa kumshauri na kumpa mbinu za kufanya.
Dk.Magufuli
 ameanza awamu ya pili ya kampeni baada ya kumaliza mikoa ya Nyanda za 
Juu Kusini na Mkoa mmoja wa Kusini wa Mtwara ambapo jana ameanza ziara 
Mkoa wa Morogoro.
 Msafara wa Mgombea
 Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama cha 
Mapinduzi,Dkt John Pombe Magufuli  ukikatiza kwenye dara la muda la Mto 
Kilombero,ambalo hutumika kupitishia vifaa mbalimbali kwa ajili ya 
ujenze wa daraja kubwa linalojengwa katika mto huo wa kilombero.
 Mgombea
 Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama cha 
Mapinduzi,Dkt John Pombe Magufuli  akikagua daraja la Mto kilombero 
ambalo ujenzi wake unaendelea mpaka sasa. 
 Mgombea
 Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama cha 
Mapinduzi,Dkt John Pombe Magufuli  akipata maelezo mafupi kuhusia na 
maendeleo ya ujenzi wa dara hilo ambalo litakuwa mkombozi mkubwa kwa 
wakazi wa Kilombero,litapunguza kero kubwa ya usafiri miongoni mwao kwa 
kiasi kikibwa.
 Baadhi ya Viongozi wa Dini wakimwombea sala  Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama cha Mapinduzi,Dkt John Pombe Magufuli  mara baada ya kumaliza kuhutubia  jioni ya leo kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika kwenye uwanja wa shule ya msingi Mahenge jioni ya leo.
 Mgombea wa Urais kupitia CCM Dk. John Pombe
Magufuli akihutubia wakazi wa Ifakara wilayani Kilombero kwenye mkutano wa
kampeni za CCM ambapo aliwaambia wananchi hao kuwa wakati wake utakuwa wa
kiutendaji zaidi ili kufanikisha maendeleo ya haraka kwa nchi na wananchi kwa
jumla.
 Wanafuatilia kwa makini yaliyokuwa yakizungumzwa kwenye mkutano huo wa kampeni za CCM jioni ya leo mjini Ifakara
 Mkutano wa kampeni za CCM ulipokuwa ukiendelea katika uwanja wa saba saba mjini Ifakara wilayani Kilombero jioni ya leo.
 Mfuasi wa CCM na bango lake
  
Wananchi wa mji wa Ifakara waliojitokeza kwa wingi kwenye mkutano wa 
kampeni za CCM ndani ya uwanja wa saba saba wilayani 
Kilombero,wakimsikiliza kwa makini mgombea Urais wa CCM Dkt Magufuli 
alipowahutubia kwenye mkutano huo.
  mgombea
 ubunge jimbo la ilombero Ndugu Abubakar Assenga almaarufu kama mtoto wa
 fundi Cherehani akizungumza jambo kwenye mkutano wa kampeni za CCM 
zilizofanyika Ifakara wilayani Kilombero jioni ya leo.
 Wananchi
 wa mji wa Ifakara walaiojitokeza kwa wingi kwenye mkutano wa kampeni za
 CCM ndani ya uwanja wa saba saba wilayani Kilombero,wakimsikiliza kwa 
makini mgombea Urais wa CCM Dkt Magufuli alipowahutubia kwenye mkutano 
huo. 
 Mgombea
 Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama cha 
Mapinduzi,Dkt John Pombe Magufuli akimkabidhi Ilani ya CCM Mgombea 
Udiwani wa CCM wilaya ya Ulanga jioni ya leo kwenye mkutano wa kampeni 
uliofanyika kwenye uwanja wa shule ya msinfi Mahenge jioni ya leo.
 Wananchi wakifuatilia hotuba ya Magufuli alipokuwa akipita kuwasalimia wananchi wa kijiji cha Lupiro-Ifakara wilayani Kilombero
nanchi wa kijiji cha Lupiro-Ifakara wilayani Kilombero wakiwa wamefunga bara bara wakimsimamisha Mgombea
 Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama cha 
Mapinduzi,Dkt John Pombe Magufuli  awasalimie alipokuwa akitokea Malinyi
Mgombea
 Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama cha 
Mapinduzi,Dkt John Pombe Magufuli akiwaaga wananchi wa mji wa Ifakara 
waliojitokeza kwa wingi kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika katika 
uwanja wa Saba saba jioni ya leo.





















Post a Comment