Mgombea
wa Urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akihutubia wakazi wa
Ifakara wilayani Kilombero kwenye mkutano wa kampeni za CCM ambapo
aliwaambia wananchi hao kuwa wakati wake utakuwa wa kiutendaji zaidi ili
kufanikisha maendeleo ya haraka kwa nchi na wananchi kwa jumla.
PICHA NA MICHUZI JR-KILOMBERO.
Wananchi wa mji wa Ifakara waliojitokeza kwa wingi kwenye mkutano wa
kampeni za CCM ndani ya uwanja wa saba saba wilayani
Kilombero,wakimshangilia kwa shangwe Mgombea Urais wa CCM Dkt Magufuli
alipowahutubia kwenye mkutano huo.
Mgombea
wa Urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akimtambulisha mgombea
ubunge jimbo la ilombero Ndugu Abubakar Assenga almaarufu kama mtoto wa
fundi Cherehani kwenye mkutano wa kampeni za CCM zilizofanyika Ifakara
wilayani Kilombero.
Mgombea wa Urais kupitia CCM Dk. John Pombe
Magufuli akihutubia wakazi wa Ifakara wilayani Kilombero kwenye mkutano wa
kampeni za CCM ambapo aliwaambia wananchi hao kuwa wakati wake utakuwa wa
kiutendaji zaidi ili kufanikisha maendeleo ya haraka kwa nchi na wananchi kwa
jumla.
MGOMBEA
urais
kwa tiketi ya CCM, Dk.John Magufuli amesema iwapo atachaguliwa katika
uchaguzi mkuu mwaka huu na kufanikiwa kuunda Serikali yake atahakikisha
baadhi
ya mambo ya msingi atayaamua kwa kupata ushauri wa marais
waliomtangulia,amesema kuwa katika kipindi hiki cha kuomba ridhaa ya
wananchi ili awe Rais hatakuwa
tayari kutoa matumani hewa ambayo anajua wazi hayatekelezeki kwani ni
dhambi na
kufafafanua kila anachoahidi anauhakika anao uwezo wa kutekeleza.
Akizungumza
kwenye mikutano yake mbalimbali ya kuomba ridhaa ya kuwania urais, Dk.Magufuli
aliwambia wananchi wa Ulanga kuwa anatambua dhamana anayoomba kwa wananchi lakini
ana uhakika malengo yake ya kuwatumikia Watanzania na kuleta maendeleo
yatafanikiwa kwani iwapo atahitaji ushaauri ataupata kwa viongozi
waliomtangulia kuongoza nchi.
Alisema
sifa kubwa ya Tanzania ni kwamba kuna viongozi wastaafu wengi wakimo marais
ambao wametanguli kuongoza nchi kuanzia awamu ya pili, ya tatu na awamu ya nne.
“Iwapo
nahitaji ushauri, wapo viongozi wengi wa kunisaidia kuniongoza .Yupo mzee Ali
Hassan Mwinyi(Rais awamu ya pili), Rais mstaafu Benjamin Mkapa, Rais Jakaya
Kikwete,Rais mstaafu Salimn Amour na Rais mstaafu Aman Abeid Karume.
“Huu
ndio utaratibu wan chi yetu kwamba wapo viongozi wa kutosha wa kunipa ushauri
katika kutekeleza majukumu yangu ya kuwatumikia Watanzania.Najua msimamo wangu
na Serikali nitakayoiunda ni kufanya kazi tu.Narudia tena kwangu mimi ni kazi
tu lakini bado ninao wazee wa kunishauri ili nifikie malengo yangu,”alisema.
Alisema
kiongozi mzuri ni Yule ambaye anaweka malengo ya kuwatumikia wananchi kwa
misingi ya uzalendo na uadilifu na anapoona kuna mambo yanahitaji ushauri kabla
ya kufikia uamuzi wapo viongozi wa kumshauri na kumpa mbinu za kufanya.
Dk.Magufuli
ameanza awamu ya pili ya kampeni baada ya kumaliza mikoa ya Nyanda za
Juu Kusini na Mkoa mmoja wa Kusini wa Mtwara ambapo jana ameanza ziara
Mkoa wa Morogoro.
Msafara wa Mgombea
Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama cha
Mapinduzi,Dkt John Pombe Magufuli ukikatiza kwenye dara la muda la Mto
Kilombero,ambalo hutumika kupitishia vifaa mbalimbali kwa ajili ya
ujenze wa daraja kubwa linalojengwa katika mto huo wa kilombero.
Mgombea
Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama cha
Mapinduzi,Dkt John Pombe Magufuli akikagua daraja la Mto kilombero
ambalo ujenzi wake unaendelea mpaka sasa.
Mgombea
Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama cha
Mapinduzi,Dkt John Pombe Magufuli akipata maelezo mafupi kuhusia na
maendeleo ya ujenzi wa dara hilo ambalo litakuwa mkombozi mkubwa kwa
wakazi wa Kilombero,litapunguza kero kubwa ya usafiri miongoni mwao kwa
kiasi kikibwa.
Baadhi ya Viongozi wa Dini wakimwombea sala Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama cha Mapinduzi,Dkt John Pombe Magufuli mara baada ya kumaliza kuhutubia jioni ya leo kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika kwenye uwanja wa shule ya msingi Mahenge jioni ya leo.
Mgombea wa Urais kupitia CCM Dk. John Pombe
Magufuli akihutubia wakazi wa Ifakara wilayani Kilombero kwenye mkutano wa
kampeni za CCM ambapo aliwaambia wananchi hao kuwa wakati wake utakuwa wa
kiutendaji zaidi ili kufanikisha maendeleo ya haraka kwa nchi na wananchi kwa
jumla.
Wanafuatilia kwa makini yaliyokuwa yakizungumzwa kwenye mkutano huo wa kampeni za CCM jioni ya leo mjini Ifakara
Mkutano wa kampeni za CCM ulipokuwa ukiendelea katika uwanja wa saba saba mjini Ifakara wilayani Kilombero jioni ya leo.
Mfuasi wa CCM na bango lake
Wananchi wa mji wa Ifakara waliojitokeza kwa wingi kwenye mkutano wa
kampeni za CCM ndani ya uwanja wa saba saba wilayani
Kilombero,wakimsikiliza kwa makini mgombea Urais wa CCM Dkt Magufuli
alipowahutubia kwenye mkutano huo.
mgombea
ubunge jimbo la ilombero Ndugu Abubakar Assenga almaarufu kama mtoto wa
fundi Cherehani akizungumza jambo kwenye mkutano wa kampeni za CCM
zilizofanyika Ifakara wilayani Kilombero jioni ya leo.
Wananchi
wa mji wa Ifakara walaiojitokeza kwa wingi kwenye mkutano wa kampeni za
CCM ndani ya uwanja wa saba saba wilayani Kilombero,wakimsikiliza kwa
makini mgombea Urais wa CCM Dkt Magufuli alipowahutubia kwenye mkutano
huo.
Mgombea
Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama cha
Mapinduzi,Dkt John Pombe Magufuli akimkabidhi Ilani ya CCM Mgombea
Udiwani wa CCM wilaya ya Ulanga jioni ya leo kwenye mkutano wa kampeni
uliofanyika kwenye uwanja wa shule ya msinfi Mahenge jioni ya leo.
Wananchi wakifuatilia hotuba ya Magufuli alipokuwa akipita kuwasalimia wananchi wa kijiji cha Lupiro-Ifakara wilayani Kilombero
nanchi wa kijiji cha Lupiro-Ifakara wilayani Kilombero wakiwa wamefunga bara bara wakimsimamisha Mgombea
Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama cha
Mapinduzi,Dkt John Pombe Magufuli awasalimie alipokuwa akitokea Malinyi
Mgombea
Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama cha
Mapinduzi,Dkt John Pombe Magufuli akiwaaga wananchi wa mji wa Ifakara
waliojitokeza kwa wingi kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika katika
uwanja wa Saba saba jioni ya leo.
إرسال تعليق