
Mwenyekiti
wa Chama cha DP,Mchungaji Christopher Mtikila ,leo asubuhi alikuwa Live
Star Tv katika kipindi cha Tuongee Asubuhi ambapo ameongelea mambo
mbalimbali kama;
Dhana ya ufisadi na aina za viongozi tunaohitaji kuwapatia Ikulu
Umuhimu wa afya bora kwa wagombea uraisi
Ahadi za CCM na CHADEMA Kutoa elimu ya bure
Mapungufu Ya Edward Lowassa.
Tafiti zilizofanywa na SYNOVATE pamoja na TWAWEZA juu ya nani ana nafasi ya kushinda uraisi
Hapo
chini kuna video za maongezi yake ambazo utapata nafasi ya
kuzisikiliza, lakini kabla ya video hizo, haya ni baadhi ya mambo
aliyoyaongea Mtikila.
1-Sababu
iliyofanya ngombea mwenza wake kutotokea ni dharura ya ugonjwa
iliyompata mkewe huko Zanzibar na amesema Jumaatatu yake alienda ofisi
za tume kufuatilia akaambiwa mwenyekiti Jaji Lubuva hajafika ofisini
anaumwa hivyo akawaambia naye jaji Lubuva kwa kushindwa kuhudhuria
ofisini kwa sababu ileile naye akatwe.
Amesema amepeleka kesi mahakama kuu na wiki ijayo ndio inatolewa uamuzi.
2.
Mtikila amesema kafungua mashtaka kuzuia Lowasa kuendelea kugombea
urais kwa hoja ya afya yake akijenga hoja kwamba muajiriwa yoyote lazima
apime afya yake hivyo lowasa anakosa sifa hiyo ya kupewa nchi.
3. Amesema watanzania tunaumwa epidomia, mwenyewe kauita ni unyani, yaani tukipewa kanga kofia viroba tunashabikia tu.
4. Amesema wanachama na viongozi wa chadema bangi na gongo kwao ni kama sakrament.
5.Amesema Lowasa ni tapeli kwa kuwa alitudanganya anaenda kutununulia mvua.
6.
Alipoulizwa nani anamuona anaweza kuibadili Tanzania kati ya Lowasa na
Magufuli alijibu magufuli ndio sahihi japo ana mapungufu yake lkn zaidi
yake yeye ndio anafaa.
Hapo chini kuna Video za Maongezi Yake
Video ya kwanza: Mchungaji Christopher Mtikila akinadi sera za chama chake
إرسال تعليق