Mwenyekiti
wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC),Jaji Mstaafu,Damian Lubuva
akizungumza na makundi maalum (hawapo pichani)jinsi watashiriki upigaji
wa kura Oktoba 25 iliyofanyika Ukumbi wa New Afrika Hoteli jijini Dar
es Salaam.
Mwenyekiti
wa Chama Shirikisho la Watu wenye Ulemavu Mkoa wa Pwani Adam Shaban
akizungumza juu jinsi ushiriki katika upigaji kura Oktoba 25 katika
mkutanao uliotishwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) uliofanyika leo
katika Hoteli ya New Afrika jijini Dar es Slaam.
Sehemu
ya washiriki wa makundi maalum katika mkutano wa NEC juu ya ushiriki
wa watu wenye ulemavu katika upigaji kura oktoba 25 uliofanyika leo
Hoteli ya New Afrika jijini Dar es Salaam.
Na Chalila Kibuda ,Globu ya Jamii
TUME
ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imesema vyama vya siasa vitangaze sera zao
kwa wananchi na sio kuingilia masuala ya utawala wa tume hiyo.
Hayo
ameyasema leo,Mwenyekiti wa tume hiyo,Jaji Mstaafu,Damian Lubuva wakati
alipokutana na makundi maalum jinsi watavyoshiriki uchaguzi mkuu
unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25 mwaka huu,amesema tume inafanya kazi
kwa mujibu wa sheria hivyo vyama vya siasa viachie tume ifanya kazi
yake.
Lubuva
amesema kuwa vyama vimekuwa vikishughulika na watu hivyo tume
itavichukulia hatua za kisheria kutokana na kukiuka kwa maadili ya
uchaguzi.
Amesema mabadiliko ya uteuzi baadhi ya watendaji NEC ni suala kawaida kutokana watu kujaza nafasi zilizoachwa wazi.
Lubuva amesema Tume haiko tayari kuingiliwa katika masuala yao ya kiutawala kutokana na kile kinachofanyika kiko katika sheria.
Amesema matokeo yatatolewa katika kila vituo na kwa mwaka watatumia siku tatu katika uchaguzi kwa matokeo yote.
Lubuva amesema wakati uchaguzi visionekane vikundi vyovyote katika eneo la kituo cha kupigia kura vikisubiri matokeo
Post a Comment