Naibu
Katibu Mkuu wa CUF Zanzibar Mhe. Nassor Ahmed Mazrui akizungumza na
vyombo vya habari kuhusiana na matukio ya miripuko ya mabomu.
Mkurugenzi
wa Mawasiliano wa Timu ya Ushindi CUF Mhe. Ismail Jussa Ladhu,
akimkaribisha Naibu Katibu Mkuu wa Chama hicho Mhe. Nassor Ahmed Mazrui
(kulia), kuzingumza na waandishi wa habari katika ofisi za Chama hicho
Mtendeni Zanzibar. (Picha na OMKR)
Na: Hassan Hamad, OMKR
Chama Cha Wananchi CUF, kimeelezea kusikitishwa na matukio ya kuwatia hofu wananchi na kuhatarisha amani ya nchi.
Akizungumza
na waandishi wa habari katika ofisi za Chama hicho Mtendeni Zanzibar,
Naibu Katibu Mkuu wa CUF Zanzibar Nassor Ahmed Mazrui, ameyataja matukio
hayo kuwa ni pamoja na miripuko inayoelezwa kuwa ni mabomu katika
maeneo ya Mkunazini na Michenzani.
Ameyataja
matukio mengine kuwa ni uvamizi uliofanywa katika kisiwa cha Tumbatu
ambao ulipelekea nyumba nne kutiwa moto na nyengine kadhaa kuvunjwa,
sambamba na kupigwa na kujeruhiwa kwa wananchi 16 wa kisiwa hicho.
Akifafanua
kuhusu matukio ya miripuko, Mhe. Mazrui ameishauri Serikali kuwatafuta
waliotega mabomu hayo kwa kutumia picha za kamera za ulinzi za CCTV
ambazo zimesambazwa katika eneo lote la Mji Mkongwe.
Amesema
bila ya kuchukuliwa kwa hatua wananchi wataendelea kuamini kuwa matukio
hayo yamepangwa makusudi kwa lengo la kuwatia hofu wananchi washindwe
kuendelea na shughuli zao za kimaisha.
Wakati
hayo yakiendelea, Mhe. Mazrui amesema juhudi kubwa zimeanza na
zinaendelea vyema kwa kuzishirikisha jumuiya na taasisi za ndani na nje
ya nchi, zikiwa na lengo la kukwamua mkwamo wa kisiasa unaoikumba
Zanzibar hivi sasa.
Nae
Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Timu ya Ushindi CUF Mhe. Ismail Jussa
Ladhu, amesema wanatiwa moyo na juhudi zinazoendelea, na kuwataka
wananchi kuendelea kuwa wavumilivu na kudumisha amani.
إرسال تعليق