Aliyekuwa mgombea Ubunge wa jimbo Ludewa, Mh Deo Filikunjombe akiwapungia wafuasi wake enzi za uhai.
Aliyekuwa
mgombea Mbunge wa jimbo la Ludewa mkoani Njombe kwa tiketi ya Chama Cha
Mapinduzi ( CCM ), Mh Deo Filikunjombe amefariki dunia.
Mh
Deo Filikunjombe amefikwa na umauti baada ya helkopta aliyokuwa amepanda
kutoka jijini Dar es Salaam kuelekea jimboni kwake kuanguka usiku wa
kuamkia leo katika mbuga ya wanyama ya Selous.
Katika
helkopta walikuwa watu wanne pamoja na rubani aliyetambuliwa kwa jina
la William Silaa ambaye naye amefariki dunia, huku watu wengine wawili
majina yao yakiwa bado hayajatambuliwa.
Rubani huyo ni baba mzazi wa Jerry Silaa ambaye anagombea Ubunge wa jimbo la Ukonga kwa tiketi ya CCM.
Mwenyezi Mungu aziweke roho za marehemu mahali pema peponi, Amina.
Nimetoka kupokea taarifa inayothibitisha kwamba chopa aliyokuwa amekodi Ndugu yetu Filikunjombe imeanguka na watu wote wamefariki.
— January Makamba (@JMakamba) October 16, 2015
Siku mbili zilizopita niliongea kwa kirefu na Deo kuhusu mikakati. Nimepoteza rafiki na ndugu. Mungu amrehemu na pole kwa familia za wafiwa.
— January Makamba (@JMakamba) October 16, 2015

إرسال تعليق