THE game
is over ! Sasa ni wazi kuwa familia ya staa mkubwa wa muziki wa kizazi
kipya Bongo, Nasibu Abdul ‘Diamond Plutnamz’ imemtema rasmi mzazi
mwenzake Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’ kwa kile wanachodai ….
“Tumechoshwa na uzungu wake”, Risasi Mchanganyiko linaweza kuandika.
Chanzo
kilicho karibu na familia hiyo kililiambia gazeti hili kuwa kina
taarifa kuwa mama Latiffa ‘Tiffah’ hatarejea tena nchini kutokana na
kushindwana na wanafamilia, kwani wanaendekeza uswahili, kitu ambacho
yeye hakiwezi.
“Familia ya Diamond ndiyo imemchoka, unajua yule hajazoea mambo ya kiswahili swahili, ametofautiana nao sana na ndiyo maana hata wao wamesema hawamtaki tena, wanahitaji mswahili mwenzao,” kilisema chanzo hicho.
“Familia ya Diamond ndiyo imemchoka, unajua yule hajazoea mambo ya kiswahili swahili, ametofautiana nao sana na ndiyo maana hata wao wamesema hawamtaki tena, wanahitaji mswahili mwenzao,” kilisema chanzo hicho.
FAMILIA YA DIAMOND HII HAPA
Ili
kujua ukweli wa maelezo hayo, mwandishi wetu alimtafuta mama mzazi wa
Diamond, Sanura Kassim ‘Sandra’ kupitia simu yake ya mkononi, na
alipoulizwa, alihamaki na kuanza kufoka, akidai hataki kuingiliwa mambo
yake ya ndani na kwamba kama kuna mtu anataka kujua zaidi amfuate Zari
huko kwao (South Afrika).
“Hata
kama ni kweli, mimi na huyo sijui Zari wenu tumegombana wewe yanakuhusu
nini? sipendi kuingiliwa kwenye mambo ya familia yangu, ninachojua ni
kwamba hayupo hapa na maisha yanaendelea,” alisema Mama Diamond na kukaa
kimya huku simu ikiwa hewani.
Wakati
simu ikiwa hewani, ghafla sauti ya kiume ilisikika na kujitambulisha
kwa jina la Anko Salum, aliyemtaka mwandishi kuachana na habari hizo,
kwani ni za ndani na zitamalizwa na wenyewe kama familia.
Wakati
mwandishi wetu akiendelea kuzungumza na Anko Salum, ghafla tena sauti
nyembamba na kali masikioni ilisikika na mwanahabari wetu akaibaini kuwa
ni ya Esma, ambaye ni dada wa Diamond.
“Mbona
mnatufuatilia sana jamani? Nani anafuatilia mambo yenu? Nafasi ya Zari
imefika mwisho, tunamkaribisha mwingine yeyote, kama kuna msichana
mrembo unamjua, tuletee nyumba yetu ni kubwa sana, na sisi tunaruhusiwa
kuoa hata wanawake wanne, Zari ameishia hapo, tena hatujagombana naye,
lakini tumechoshwa na uzungu wake, awamu hii tunahitaji mswahili
mwenzetu.
“Zari
ameenda kwao, kulea watoto wake na kuangalia ustaarabu mwingine,
tunamtakia kila la kheri, lakini hatuna ugomvi naye kabisa,” alisema
Esma.Jitihada za kumpata Diamond hazikuzaa matunda kutokana na namba
yake ya mkononi kutokuwa hewani kila alipopigiwa, hata hivyo jitihada
zaidi zinaendelea kumtafuta
Post a Comment