Usiku wa October 21 michezo ya Ligi ya Mabingwa Ulaya iliendelea tena kwa michezo nane kupigwa katika viwanja mbalimbali barani Ulaya.
Usiku wa October 21 ilipigwa michezo nane kutoka katika timu zilizomo
katika Makundi A, B, C na D. Makundi ambayo yana timu za Real Madrid na Paris Saint Germain.
Mchezo wa Kundi A uliyokuwa unazikutanisha timu za Paris Saint Germain ya Ufaransa dhidi ya Real Madrid ya Hispania ulikuwa ni mchezo ambao ulivuta hisia za watu wengi, mchezo huo ambao ulipigwa katika dimba la Parc des Princes nchini Ufaransa, ulimalizika kwa timu zote mbili kutofungana na kuishia kwa sare ya 0-0.
Vilabu vya Real Madrid ya Hispania na Paris Saint Germain ya Ufaransa vina wachezaji mastaa kama Cristiano Ronaldo na Zlatan Ibrahimovic
hivyo wengi walitegemea kuona mastaa hao wakifunga magoli mengi ila
mambo yamekuwa tofauti kwa nyota hao kushindwa kutamba kwa kupachika
goli na mchezo kumalizika kwa sare ya kutofungana magoli.
Video za magoli ya mechi ya CSKA Moscow Vs Manchester United
Video za magoli ya Manchester City Vs Sevilla



إرسال تعليق