Sta wa sinema za kibongo, Blandina Chagula maarufu kama Johari.
MAYASA MARIWATA
BLANDINA Chagula maarufu kama Johari,
ambaye ni mmoja wa wasanii wanaozunguka nchi nzima kuipigia kampeni CCM
katika uchaguzi mkuu, amesema baada ya kutembea na kufanya kazi,
amejikuta akiihamishia akili yake katika siasa.

“Kuna
wakati nilikuwa naafikiana na yale madai kuwa serikali haijafanya
lolote, lakini baada ya kuzunguka katika mikoa mbalimbali, nimejionea
maendeleo yaliyopo na nimejifunza mambo mengi, nimepata hamasa kubwa ya
kuingia kwenye siasa na huenda nikagombea ubunge uchaguzi ujao,” alisema
muigizaji huyo wa siku nyingi.

Aidha,
alisema alipokuwa Dar alizoea kuamka wakati wowote aliotaka, lakini
ratiba za hivi sasa zimemfanya kuwa fiti zaidi kwa sababu ni kazi tu
kuanzia asubuhi hadi jioni wakipita nyumba hadi nyumba, mtaa hadi mtaa
jambo lililomfanya kubadilika kwa mambo yake mengi.

Post a Comment