
MABADILIKO! Baada ya kunusurika kwenye
vifo vya mkanyagano vilivyoua mahujaji zaidi ya 4000 waliokwenda kuhiji
katika mji wa Mina, Makka nchini Saudi Arabia, staa wa filamu za Bongo,
Amri Athuman ‘Mzee Majuto’ amerejea salama akiwa shavu dodo na kusema
ameachana na maisha ya zamani, sasa amekuwa mtu wa tofauti kabisa.
Akizungumza na Risasi Mchanganyiko
katika mahojiano maalum mara baada ya kuwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa
Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) Jumamosi iliyopita na kupokewa
kifalme, kwani mamia ya ndugu waliofika uwanjani hapo kuwapokea mahujaji
wengine, walitaka kumpa mkono na kupiga picha na staa huyo wa
vichekesho nchini .

….Akipokelewa na ndugu zake.
SANAA BASI?
Alisema: “Nimerudi salama jamani. Lakini
nimejifunza mengi sana kule Makka. Tamko langu kubwa kuhusu sanaa ni
kwamba, sitacheza tena filamu zinazohusu mapenzimapenzi wala kushiriki
matangazo ya kwenye runinga yenye mwelekeo wa mapenzi. Sitaingia tena
baa. Pia masuala ya wasichana ‘dogodogo’ ambao wamezoea kunishobokea
wanatakiwa wapite mbali na mimi.
“Lakini pia kuna hii tabia ya wasichana
kutaka kupiga picha na mimi kwa kutumia simu za Smart Phone, wenyewe
mnaita ‘selfie’ sitaki kwani mambo yote hayo ni chukizo kwa Mwenyezi
Mungu na yatanirudisha nilikokuwa zamani, sitaki nitoke kwenye maisha
yangu ya sasa yaliyobaki hapa duniani.”

Mzee Majuto alikwenda mbele zaidi kwa
kusema kwa sasa ataishi maisha ya kitakatifu zaidi, ambapo kwa mwezi
atatumia siku kumi kusafiri sehemu mbalimbali za nchi kwa ajili ya
kuwafundisha watu mafundisho ya Mwenyezi Mungu.
“Ukweli sasa nimekuwa mtu wa ibada kila
mara. Kama ni filamu nitacheza zile ambazo hazimchukizi Mwenyezi Mungu.
Na muda mwingi nitawafundisha watu mafundisho ya Mwenyezi Mungu. Nikiona
sanaa inaniingiza majaribuni nitaachana nayo kabisa kwani tayari
nimeshajenga msikiti na madrasa kule Tanga,” alisema Mzee Majuto.
AOMBA AOMBEWE
Alisema: “Mimi ni binadamu, hivyo kwa
nguvu zangu na akili zangu sitaweza kuyatimiza hayo, hivyo nawaomba
Watanzania waniombee ili niishi maisha ya kumpendeza Mwenyezi Mungu na
nisirudi kule nilikokuwa zamani.”
ALIVYONUSURIKA KUFA MAKKA
Aidha, Mzee Majuto alianika jinsi yeye na mahujaji wengine walivyofanikiwa kumaliza ibada ya hija salama Makka na mahujaji wote wakaelekea kwenye kutimiza nguzo tano za Kiislamu za kumpiga mawe shetani Mina ambako huko ndiko maafa ya kukanyagana yalitokea.
Aidha, Mzee Majuto alianika jinsi yeye na mahujaji wengine walivyofanikiwa kumaliza ibada ya hija salama Makka na mahujaji wote wakaelekea kwenye kutimiza nguzo tano za Kiislamu za kumpiga mawe shetani Mina ambako huko ndiko maafa ya kukanyagana yalitokea.
Alisema: “Nilikuwa tayari kwenda Mina
lakini kilichoninusuru nisiende, mimi nina tatizo la goti hivyo kwenda
huko nilishindwa, nikamuomba mtu akanisaidie kunirushia jiwe langu la
kumpiga shetani, mimi nikabaki hotelini. Lakini baada ya muda mfupi
alirudi na kuniambia hali ni mbaya na mahujaji wengi wamekufa kwa
kukanyagana.
“Ila kwa unene wangu huu, naamini kama ningekuwa miongoni mwa watu waliokwenda Mina kumpiga shetani, huenda ningekanyagwa na kufa.”
“Ila kwa unene wangu huu, naamini kama ningekuwa miongoni mwa watu waliokwenda Mina kumpiga shetani, huenda ningekanyagwa na kufa.”
ILIKUWAJE?
Kwa mujibu wa Mzee Majuto, vifo hivyo
vilitokea kwa sababu ya kufungwa kwa njia moja kati ya mbili za
kuingilia Mina kutokana na matumizi ya kifalme, ikabidi itumike njia
moja kinyume na utaratibu ambapo idadi ya mahujaji waliokuwa wanakwenda
na wanaorudi ilikuwa kubwa
Post a Comment