Asakari polisi na wataalamu wakikagua mabaki ya chopa
namba 5Y-DKK iliyoanguka jana jioni ikitokea Dar kuelekea Ludewa
sehemu ya hifadhi ya wanyama ya Selous ambapo Mbunge wa Ludewa Deo
Filikunjombe, rubani Capt. William Slaa na abiria wengine wawili -
Casablanca Haule na Ngondombwitu Nkwera - walipoteza maisha.
Timu ya waokoaji wakibeba mabaki ya miili ya marehemu
Askari wakiwa eneo la ajali
Mbunge
wa Ludewa Mhe Deogratias Haule Filikunjombe (chini) amefariki dunia
katia ajali ya Chopa katika hifadhi ya wanyama ya Selous, pamoja na
rubani Kepteni William Silaa (juu kulia), mfanyakazi wa halmashauri ya
wilaya ya Ludewa na ndugu yake Marehemu Filikunjombe ambao majina
hayajapatikana mara moja.
Mhe.
Deo Filikunjombe, rubani na na abiria wengine walipata matatizo ya
engine ya chopa namba 5Y-DKK jana jioni wakitokea Dar kuelekea Ludewa.
Kwa
mujibu wa Meya wa Ilala aliyemaliza muda wake Mhe Jerry Silaa, ambaye
ni mtoto wa rubani, hakuna mtu aliyenusurika katika ajali hiyo ya
Chopa.
"Kwa
masikitiko makubwa nimepokea taarifa rasmi kutoka kwa timu ya uokoaji
kuwa imefanikiwa kufika eneo la ajali na kukuta abiria wote na rubani
wamepoteza maisha.
"Ni mepoteza Baba na rubani mzuri wa nchi yetu Capt. William Silaa.
Nimepoteza
rafiki na kiongozi wangu Mhe. Deo Filikunjombe. Nawapa pole wote
waliopoteza ndugu zao. Nawaombea marehemu mapumziko ya Amani.
Nawashukuru wote walioshirikiana na familia kusaidia uokozi", amesema
Mhe Jerry Silaa katika kurasa zake za mitandaoni.
tangia
jana habari za kuanguka kwa nchopa hiyo zilitapakaa kila kona na katika
mitandao, na kuendelea hadi leo tangia asubuhi hadi baada ya ujumbe wa
Jerry Silaa kupatikana mchana huu.







إرسال تعليق