NI ICJ SIO ICC.!
Kuna watu wamekua wakihoji iweje viongozi wa UKAWA waende ICC wakati
hakuna makosa yoyote ya uhalifu wa kivita yaliyotokea nchini? Wengi
wanaoongea hivi ni CCM na wanaonekana wazi kuwa wako missinformed. Mara
nyingi CCM huwa wanajenga hoja bila kuwa na taarifa za kutosha. (Elimu,
Elimu, Elimu).!
Jibu sahihi ni kwamba viongozi wa UKAWA hawajaenda ICC wameenda ICJ.
Hizi ni mahakama mbili tofauti zenye jurisdiction tofauti japo zipo mji
mmoja wa The Hague.
The Hague kuna mahakama mbili. Ya kwanza ni mahamaka ya uhalifu wa
kivita na makosa yatokanayo na vita vya kisiasa (Internation Criminal
Court au ICC kwa kifupi). Ya pili ni mahakama ya kimataifa ya haki za
raia (International Court of Justice, au ICJ kwa kifupi).
So kina Mbowe wameenda ICJ sio ICC. Wangeenda ICC ikiwa Serikali
ingehusika na mauaji ya raia wakati wa uchaguzi. Lakini kwa kuwa hakuna
uhalifu wa kivita uliotokea thats why wameenda ICJ.
ICJ inashughulikia mambo mengi ikiwa ni pamoja na issues za malalamiko
ya uchaguzi. Kwa mujibu wa Article 93 ya UN Charter, nchi zote wanachama
wa UN ni member wa mahakama hii. Na raia wa nchi hizo wanaweza kufile
kesi kuhusiana na ukiukwaji wa haki za raia katika nchi zao, ikiwa ni
pamoja na mambo ya uchaguzi.
KWANINI ICJ?
Iko hivi wakati tunavunja mkataba wa Richmond tulishtakiwa ICJ
tukashindwa kesi na hadi leo tunalipa hasara iliyotokana na kuvunja
mkataba ule. Na sio Richmond tu zipo kesi nyingi tumewahi kushtakiwa ktk
mahakama za kimataifa na tukashinda au kushindwa na tukatekeleza hukumu
iliyotolewa.
Hivyo basi ili kulinda amani ya nchi Lowassa amefungua kesi ktk mahakama
hiyo kudai kuporwa ushindi. Jana ametakiwa kupeleka "documents" za
kudhibitisha madai yake na zilipelekwa jana na jopo la mawakili wa chama
akiwemo John Mallya.
Kutokana na vielelezo vya Chadema, mahakama hiyo ilijiridhisha kuwa kuna
kesi ya kujibu. Hivyo imewaagiza CCM nao kupeleka vielelezo vyao
vinavyoonesha kuwa wameshinda kihalali (yani nakala zote za fomu za
matokeo ktk majimbo ya uchaguzi kama ilivyofanya UKAWA).
Leo CCM imepeleka jopo la mawakili nchini Uholanzi kwa ajili ya
kuwasilisha utetezi wake. UKAWA nao wataongeza mawakili wengine jioni ya
leo akiwemo Tundu Lissu.
Tume ya Uchaguzi (NEC) kama sehemu ya walalakiwa ktk shauri hili nayo
itawasilisha utetezi wake mbele ya mahakama hiyo chini ya jopo la majaji
watatu kutoka serikalini.
Taarifa zisizo rasmi zinasema kesi hiyo itaanza kusikilizwa kesho na
hukumu kutolewa kabla Rais mpya wa Tanzania hajaapishwa (November 05).
Pamoja na mambo mengine mahakama hiyo itapitia upya fomu zote za matokeo
ktk majimbo yote kutoka NEC pamoja na zile zilizowasilishwa na CHADEMA
na CCM ili kubaini kama kulikua na udanganyifu.
NB;
Mahakama hii haina mandate ya kumvua Magufuli ushindi (kuyokana na
Katiba yetu ibara ya 41(7) kuzuia. Ila jurisdiction ya Mahakama hii ni
kusema kama kuna udanganyifu ulifanyika au lah. Mahakama hii pia inaweza
kueleza kama kuna njama za kuhujumu matokeo (conspiracy) zilizofanywa
baina ya CCM na Tume ya Uchaguzi. Kwahiyo hata km mahakama hii haiwezi
kumvua Magufuli ushindi, lakini hukumu yake inaweza kusababisha uchaguzi
urudiwe kama ilivyofanya kwa nchi ya Romania miaka iliyopita.
MY TAKE.!
Hii imedhihitisha kuwa Lowassa ni kiongozi wa kipekee (Charismatic
Leader). Anajua watu wana uchungu na ubakaji wa demokrasia uliotokea.
Anajua neno lake moja tu linaweza kufanya mamilioni ya watanzania
wakakusanyika barabarani bila kuhofia kupoteza maisha yao. Anajua kuwa
ana nguvu na uwezo wa kuitisha maandamano nchi nzima na vyombo vya dola
vikashindwa kuzuia hata vikiua baadhi. Anajua kwa nguvu aliyonayo
anaweza kupelekea taifa hili likaingia kwenye machafuko makubwa.
Lakini badala ya kufanya hivyo ameamua kutumia njia za kistaarabu kudai
haki yake. Ameamua kwenda Mahakamani. Kwangu hii ni sifa ya kiongozi
bora wa karne. Naanza kuelewa kwanini alisisitiza ELIMU, ELIMU, ELIMU.
Lowassa anapenda Elimu, anatamani watu wapate Elimu, Lowassa anaiishi
Elimu. May GOD in Trinity bless him abundantly.!
Chanzo...Jamii Forum
Post a Comment