Estomih Millah enzi za uhai wake.
…Akihutubia kwenye moja ya mikutano yake ya kampeni.
MGOMBEA Ubunge wa Jimbo la Arusha Mjini kwa tiketi ya Chama cha ACT Wazalendo, Estomih Millah amefariki dunia usiku wa kuamkia leo katika hospitali ya rufaa ya KCMC.
Ndugu Malla alipelekwa hospitali ya KCMC jana mchana akitokea Hospitali ya St. Thomas iliyopo Arusha Mjini baada ya kulazwa kwa siku mbili baada kupatwa na tatizo la shinikizo la damu.
Hali hiyo ilimtokea Oktoba 6, mara baada ya kumalizika mkutano wa kampeni uliokuwa unafanyika Ngaramtoni, Malla alilalamikia kuhisi kizunguzungu na baadae kupelekwa hospitali ya St. Thomas ambapo madaktari walisema ndugu Malla anasumbuliwa na uchovu na hivyo anatakiwa kupumzika kwa muda mrefu.
Kwa mujibu wa Ofisa Habari wa Chama cha ACT Wazalendo, Abdallah Khamis, amethibitisha kutokea kwa kifo hicho na kwamba marehemu alifariki usiku wa kuamkia leo Oktoba 9, 2015 saa saba usiku.
Amesema taarifa zaidi zitatolewa baadae baada ya uongozi wa chama hicho kufanya mawasiliano na viongozi waliopo mkoani Arusha

إرسال تعليق