Katibu wa Chama cha
Mapinduzi CCM Mkoa wa Mwanza Miraji Mtaturu (Pichani) amesema kuwa
maandalizi kwa ajili ya shughuli ya kufunga kampeni za Uchaguzi Mkuu
kitaifa kwa upande wa Chama hicho inayotarajiwa kufanyika hii leo katika
Uwanja wa CCM Kirumba yamekamilika.
Na:George Binagi-GB Pazzo
Screen kubwa itafungwa nje ya
uwanja huo kwa ajili ya wale watakaokosa nafasi ya kuingia uwanjani kwa
kuwa shughuli hiyo inatarajiwa kuhudhuriwa na maelfu ya wakazi wa Jiji
la Mwanza na Maeneo jirani.
Mbali na Mgombea Urais wa
CCM Dkt.John Pombe Magufuli kuwepo katika mkutano huo, pia Mwenyekiti wa
CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania anaemaliza muda wake
Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete anatarajiwa kuwa miongoni mwa viongozi
watakaohudhuria katika Mkutano huo wa Ufungaji wa Kampeni za Uchaguzi
Mkuu kwa upande wa CCM.
Wakati Watanzania
wakitarajia kushiriki zoezi la Uchaguzi Mkuu siku ya kesho jumapili ya
Octoba 25, Chama cha Mapinduzi CCM kimejihakikishia ushindi mnono katika
maeneo mbalimbali nchini kuanzia ngazi ya udiwani, Ubunge na Urais.
Shamra shamra kwa makada wa
CCM zimepamba moto katika maeneo mbalimbali ya Jiji la Mwanza katika
kuelekea kwenye ufungaji wa kampeni za chama hicho kitaifa unaofanyika
katika Uwanja wa CCM Kirumba.
Post a Comment