Anasema kamati kuu haiwezi kusema watu watano au sita ni
hawa bila kuwasikiliza, kilichotokea mwaka huu ni tofauti kabisa
kilichotokea mwaka 1995, safari mwenyekiti ni Jakaya Kikwete,
kilichotokea ni jambo kubwa katika historia yetu na mimi katika historia
yangu pale ambapo naona kwamba katiba inavunjwa nimekuwa na tabia ya
kusema waziwazi na kuwaambia wenzangu si sawa.
Mwaka 1972 nikiwa mkuu wa mkoa Simiyu, kulikuwa na Bunge Dar es Salaam,
nikakuta kuna mswada wa kurekebisha katika kuhusiana na swala la wakuu
wa mikoa. Mchango wangu uliibua hisia kali na kumwambia mwenyekiti
muswada aurudishe maana hatuukubali, kwa upande wa watu walipo
serikalini walisema ndio na wabunge wa kuchaguliwa walisema hapana.
Ilipofika zamu yangu nikasema sina upande, wabunge walifurahi sana. Kura
zilipohesabiwa serikali ilishindwa kwa mara ya kwanza katika mfumo wa
serikali ya chama kimoja. Mzee Kawawa aliniita akasema wewe ni mwenzetu
lakini umetuacha, Rais atakubadilisha kazi.
Nilipoitwa na mwalimu nilimueleza kwa nini nilikataa na akasema
ningekuwa katika nafasi yako ningepinga lakini mimi ndio naongoza nchi
lakini usiwe na wasiwasi. Tukakubaliana na siku ya pili nikatangazwa
nimeachishwa uwaziri. Nilifanya uamuzi ule nikijua kabisa naweza
kupoteza kazi lakini kwenye masula ya kimsingi huwa sitetereki.
Mimi sikubaliani na mambo yaliyotokea tarehe kumi na kumi na moja
Dodoma, kilichotokea ni kuwadhalilisha wagombea wenye haki, kamati kuu
ingeweza kuwahoji na kuamua. Hili halikfanyika. wadhalilishwa,
wamezungushwa mikoa 15 kwa gharama zao na kuishia mlangoni mwa kamati
kuu.
CCM inaamini binadamu wote ni sawa na kila mtu anastahili heshma ya
kutambuliwa utu wake, kuwazungusha alafu nyinyi mmefunga mlango, si
kuwadhalilisha? Katika nchi yetu hao waliodhalilishwa wamenyamaza moja
kwa moja isipokuwa Mwandosya, aliinuka na kusema kwamba kweli
wamedhalilishwa na kadhalika.
Nawapongeza Kimbisa, Sophia na Nchimbi kwa kueleza yaliyotokea kamati
kuu, tuliingia chama hiki si kwa ajili ya kutafuta cheo na wengine
tuliacha kazi kwa mkoloni. Tulitafuta chombo cha ukombozi kwa watanzania
na waafrika.
Kwa kuwa uongozi wa sasa wa chama cha mapinduzi kufanya yale wanayotaka
wao kwa maslahi ambayo sina hakika ni ya nani, vijana wanatumiwa
kudhalilisha watu wazima, watu wanaajiriwa kutukana tu watu, mimi nasema
sikubaliani na hiko sio chama tulichoshirikiana kukijenga.
Mimi kuanzia leo naachana na chama cha mapinduzi kwa sababu siwezi
kuhimili chama kinachoendeshwa bila kuheshimu katiba kwa sababu katiba
ndio inayotuunganisha sisi sote. Sasa nasema kuanzia sasa najitoa chama
cha mapinduzi, najua uamuzi wangu utasumbua baadhi ya rafiki zangu,
makada wenzangu na wazee wenzangu hata vijana lakini ni uamuzi ambao
lazima niufanye kwa sababu vinginevyo mimi nitajisaliti mwenyewe.
Nimehusika kuweka misingi ya chama chetu, ndani ya chama chetu kumekuwa
na demokrasia halafu wakuu wanakwenda kutangaza kwenye majukwaa hakukuwa
na tatizo lolote, mambo yote yalikuwa sawasawa.
Sikusudii kujiunga na chama kingine chochote na nina sababu, mimi
nimekuwa mwanaharakati wa TANU na CCM kwa muda wa miaka 61, nadhani
miaka 61 inatosha mimi kuwa mwanaharakati.
Tatu mimi ni raia tena raia huru wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania,
nna haki zangu za kisisasa na kijamii hivyo nitaendelea misimamo yangu.
Katika hali ya sasa ina makundi mawili, moja linasema kidumu chama
tawala maana yake hakuna mabadiliko. Kundi jingine linasema linataka
mabadiliko katika nchi yetu, sitaki kusema kundi lipi kubwa lakini
nasema hali iko hivyo, kwa jinsi nnavyotazama vijana wanataka mabadiliko
ukiondoa vijana wangu wa UVCCM, kina mama walio wengi wanataka
mabadiliko, wafanyakazi wakulima, wafugaji, wavuvi, wachimba migodi
wadogowadogo najua wengi wao wanataka mabadiliko, wanafunzi hasa wa
sekondari ya juu, wa vyuo na vyo vikuu na wasomi wa nchii walio wengi
wanataka mabadiliko.
Nilisema siku moja nilipoulizwa nani unamuona anafaa kugombea Urais,
niliwaambia kwamba mimi nitamuunga mkono yule ambae ziko dalili zote
wananchi wanasema ndie anaefaa. Pia nilisema nilipokuwa na ndugu Lowassa
Arusha, Mwalimu alisema ulizeni wananchi wanasema nini?
Katika hili swala la mabadiliko mimi niko upande wa mabadiliko tena mimi
nasema wamechelewa, walio wengi wanataka mabadiliko. Mimi nasema niko
upande wa mabadiliko kwa sababu ya wale. Katika historia yetu katika
TANU na Afro shirazi sisi tulikuwa upande wa mabadiliko.
Tuliungana na hio ilikuwa mabadiliko, mwaka 77 tuliua Afro Shirazi, tuliua TANU na kufanya mabadiliko.
Baada ya kukaa madaraki miaka mingi hatuwezi kuleta jipya pamoja na
ahadi za Magufuli, nusu karne ni muda mrefu sana, pumzi, kuongoza nchi
na kama kupanda mlima, unafika mahala pumzi zinakwisha, huwezi kuendelea
mbele na ukitaka kuendelea wananchi wanabaki palepale walipo.
Tatizo la wananchi ni uchumi, ajira, sasa umasikini unaondolewa na uchumi imara.
Mkapa alitufanyia kazi nzuri kwa kututoa kwenye ukuaji wa asilimia 3
mpaka 4, wakati anakabidhi madaraka ulikuwa unakuwa kwa 7%. Kikwete
amepokea madaraka unakuwa kwa 7%, sasa miaka kumi baadae uchumi unakuwa
kwa 7%. Maana yake miaka kumi hii tumepiga maktaimu, tumebaki palepale
maana yake ni kurudi nyuma.
Idadi ya watu imeongezeka, midomo imeongeza, miguu imeongezeka lakini
ukuaji uko palepale, bei ya sukari kwa mfano ni ya kuruka, bei ya sukari
Mkapa aliacha 600 sasa inaenda 2000. Nini! Pumzi. Kwenda kwenye maisha
bora kunataka pumzi.
Tulianza na maisha bora kwa kila mtanzania lakini sasa hatusemi tena
habari hizo, mabadiliko ni muhimu kwelikweli, tupate pumzi mpya. Mnataka
mbaki nyinyi tu, nyinyi pumzi imekwisha. Chama kifutike? Hapana lakini
kiwekwe benchi kidogo kijitafakari.
Kama hamjadili mambo mtapata wapi mawazo ya kwenda mbele, lazima ukuaji
wa uchumi wa nchi angalau ufike 10%. 7% mpaka 10% si mbali lakini miaka
kumi tuko palepale. Wachina wamekuwa wakikuza uchumi wao mpaka asilimia
15 na zaidi, na sisi hapa baadhi yetu kama watu watakuwa wanyenyekevu
kupata mawazo ya wenzao tutapiga hatua.
Mimi nimekuwa mwenyekiti wa ilani zote za uchaguzi kasoro moja tangu
mwaka 90, tatizo la ajiri kwa vijana linaonekana kana kwamba
halitatuliki wakati linatatulika, kujiajiri na kutoa mitaji. Wanaotaka
kujidanganya kwamba wataleta mabadiliko haya!
Lakini tunaotaka kwenda mbele, kung'ang'ania kwamba lazima wao wawe madarakani mtakuja kujilaumu wenyewe siku moja.

إرسال تعليق