TANZANIA
imetimiza ndoto za kutinga hatua ya mwisho ya mchujo kuwania kupangwa
kwenye makundi ya kuwania tiketi ya Fainali za Kombe la Dunia, licha ya
kufungwa 1-0 na Malawi jioni ya leo katika Uwanja wa Kamuzu mjini
Blantyre.
Tanzania
inasonga mbele kwa ushindi wa jumla wa 2-1, baada ya Jumatano kushinda
2-0 Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam katika mchezo wa kwanza wa hatua ya
kwanza ya mchujo.
Katika
mchezo huo uliochezeshwa na refa wa Angola, Martins de Carlvalho
aliyesaidiwa na Gadzikwa Bongani wa Zimbabwe na Valdmiro Ntyamba wa
Angola, hadi mapumziko Malawi walikuwa mbele kwa bao hilo 1-0,
lilifungwa na John Banda dakika ya 42 aliyefumua shuti kali akimalizia
pasi ya Chiukepo Msowoya.
Taifa
Stars ndio walioanza mchezo huo kwa kasi na dakika ya kwanza tu,
mshambuliaji Mbwana Samatta alikaribia kufunga, baada ya kumtoka beki
Limbikani Mnzava, lakini kipa Simplex Nthala akaokoa.
Malawi
wakajibu shambulizi dakika ya pili baada ya shuti kali la Banda
kupanguliwa na kipa Ally Mustafa ‘Barthez’. Barthez akafanya kazi nzuri
tena dakika ya 10 baada ya kuokoa michomo miwili mfululizo ya Malawi.
Stars
ilizinduka dakika ya 35 baada ya Thomas Ulimwengu kumtoka vizuri beki wa
Malawi Yamikani Fodya baada ya pasi ndefu ya Samatta, lakini shuti lake
likaenda nje sentimita chache.
Kipindi
cha pili, kocha wa Stars, Charles Boniface Mkwasa alianza na
mabadiliko, akimtoa kiungo Said Ndemla na kumuingiza mshambuliaji John
Bocco.
Mabadiliko
hayo yaliifanya Stars ianze kudumu kwenye eneo la Malawi, lakini bado
mashambulizi ya hatari yalielekezwa langoni mwa Tanzania.
Dakika
ya 58 Nahodha wa Tanzania, Nadir Haroub ‘Cannavaro’ aliokoa hatari
langoni mwake na dakika ya 62 Malawi walifanya mashambulizi matatu
mfululizo ya hatari lanoni mwa Stars, ikiwemo kupata kona mbili.
Dakika ya 72 Mbwana Samatta alipiga shuti hafifu akiwa karibu na lango baada ya kupokea pasi nzuri ya John Bocco likaenda nje.
Malawi walifanya shambulizi la hatari dakika ya 90, lakini Robin Ngalande akashindwa kumalizia vizuri baada ya kupiga nje.
Kwa matokeo hayo, Taifa Stars sasa itamenyana na Algeria katika mechi za mwisho za mchujo mwezi Novemba.
Kikosi
cha Tanzania; Ally Mustafa ‘Barthez’, Shomary Kapombe, Mwinyi Hajji,
Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Kevin Yondan, Himid Mao, Thomas Ulimwengu,
Said Ndemla/John Bocco dk46, Mudathir Yahya, Mbwana Samatta na Farid
Mussa/Mrisho Ngassa dk75.
Malawi;
Simplex Nthala, Stanley Sanudi, Miracle Gabeya/Robin Ngalande dk76,
Yamkani Fadya, Limbikani Mzava, Gerald Phiri, Chimango Kayira, Micium
Mhone, Chiukepo Msowoya, John Banda na Shumaker Kuwali.
Post a Comment