SERIKALI
imeshauriwa kuutumia vema mwezi Oktoba, mwaka huu kukuza uelewa kwa
wananchi juu ya masuala ya mitandao ili kupunguza kama si kuondoa kabisa
uhalifu mitandaoni.
Rai
hiyo ilitolewa jana jijini Dar es Salaam na Mtaalamu wa Usalama wa
Mitandao na Uchunguzi wa Makosa ya Kidijitali, Yusuph Kileo wakati
akizungumza na Majira.
"Nichukue nafasi hii kutambua na
kuhamasisha tukio la kipekee katika anga ya usalama katika mitandao
jambo ambalo limekuwa likiadhimishwa kila mwaka katika mwezi wa Oktoba,
ambapo mataifa yanaadhimisha siku ya uelewa wa masuala ya usalama wa
mitandao duniani kote," alisema Kileo.
Alisema,
wakati mataifa mbalimbali duniani yakitarajiwa kuadhimisha tukio hilo
anaamini Tanzania itauchukulia mwezi huo kinamna ya kipekee ili kuweza
kukuza uelewa kwa watu wake. Hilo
ni tukio ambalo nategemea kampuni mbalimbali na maeneo mengine
yataandaa programu mbalimbali za kukuza uelewa wa masuala ya usalama
mitandaoni ili kuweza kufikia malengo yaliyokusudiwa na wanausalama wote
wa mitandao duniani kote," aliongeza mtaalamu huyo.
Aidha,
alisema inaaminika kama ilivyo katika uhalifu mwingine wowote kuwa ni
vigumu kumaliza kabisa tatizo ila kuna njia kadhaa ambazo kwa umoja wake
zikifanyiwa kazi vizuri zinaweza kabisa kupunguza kwa kiasi kikubwa
tatizo la uhalifu kwenye mitandao.
"Tatizo
kubwa ni kuwa njia hizi zimekuwa zikiishia katika maandishi baada ya
kujadiliwa na wanausalama wa mitandao; mimi binafsi nilikuwa miongoni
mwao," alifafanua Kileo.
Alisema,
baadhi ya njia za kukabiliana na tatizo hilo ni kupitia elimu ya
uelewa wa uhalifu katika mtandao na namna ya kujilinda.
"Elimu
hii inatoa fursa kwa mwananchi wa kawaida kutambua aina mbalimbali za
uhalifu kwenye mitandao, athari zake, njia ya kujilinda na namna ya
kulinda wenzake," alisema Kileo.
KUPITIA
KIPINDI CHA KUMEPAMBAZUKA CHA RADIO ONE NIMEPATA KUSHIRIKI KWA NJIA YA
SIMU HOJA ILIYO HOJI ---- IKIWA NI TAKRIBANI MWEZI MMOJA BAADA YA KUANZA
KUTUMIKA KWA SHERIA YA MAKOSA YA MTANDAO HAPA NCHINI,WIZARA YA
MAWASILIANO,SAYANSI NA TEKNOLOJIA PAMOJA NA WADAU WENGINE WANATOA
TATHIMINI GANI.
إرسال تعليق