Katika
kuimarisha maandalizi ya Timu ya Taifa (Taifa Stars) kuelekea katika
mashindano mbalimbali ikiwemo mechi mbili za ugenini na nyumbani dhidi
ya Algeria, Rais wa TFF Jamal Malinzi ameunda kamati maalum itakayoitwa
“Kamati ya Taifa Stars” ambayo majukumu yake yatakua:
(i) Kuimarisha huduma kwa wachezaji,
(ii) Uhamasishaji na Masoko,
(iii) Kuhamasisha wachezaji,
(iv) Kuandaa na kusimamia mkakati wa Ushindi.
Kamati hii itaongozwa na Mwenyekiti Farough Baghouzah, Teddy
Mapunda (Katibu), Wajumbe ni Juma Pinto, Michael Wambura, Iman Madega,
Salum Abdallah na Isaac Chanji.
Aidha Kamati hiyo imepewa jukumu la kuwashirikisha wadau mbalimbali wa mpira wa miguu katika kutekeleza majukumu hayo.
Wadau wa mpira wa miguu
ambao kamati itashirikiana nao ili wajumuike na kusaidia majukumu
mbalimbali katika kamati hiyo wanaombwa waitikie wito huo
إرسال تعليق