NI
gumzo! Ubuyu motomoto ambao unasambaa kwa kasi ya ajabu kama moto wa
kifuu mjini unadai kuwa, staa nambari moja Bongo Fleva, Nasibu Abdul
‘Diamond Platnumz’ na mwigizaji Kajala Masanja wamedaiwa kuwa ni wapenzi
na sasa ni mahaba niue, Risasi Jumamosi limesheheni full stori.
TUJIUNGE NA CHANZO
Kwa
mujibu wa chanzo makini, uhusiano wa Diamond na Kajala unadaiwa
kuibuka ghafla miezi kadhaa iliyopita lakini wamekuwa wakifanya siri
nzito kabla ya hivi karibuni kukolea zaidi baada ya mpenzi wa Diamond,
Zarina Hassan ‘Zari The Boss Lady’ kurudi nchini mwake, Afrika Kusini
‘Sauz’.
“Walianza
zile za kimjinimjini, wakawa wanafanya yao kimyakimya tangu Zari
akiwepo lakini mahaba niue yamekuja kushamiri zaidi baada ya Zari
kutimkia zake Sauz,” kilisema chanzo chetu.
MASTAA WAZUNGUMZIA
Mara
baada ya chanzo hicho kumwaga ubuyu huo, Risasi Jumamosi lilipenyezewa
data kutoka kwa mastaa tofauti ambao wanafahamu uhusiano huo mpya ambao
pia ulianza kusambaa taratibu katika mitandao ya kijamii.
“Hivi
kwani nyinyi hamjaipata habari hii? Diamond amemnasa Kajala na mambo
yao ni bambam. Sema kiukweli Diamond ni msiri maana unajua ana mambo
mengi hivyo hapendi kabisa hii ishu ijulikane,” alisema staa mmoja
mkubwa Bongo huku akiomba hifadhi ya jina.
Kama
hiyo haitoshi, staa mwingine aliliambia Risasi Jumamosi kuwa, dada wa
Diamond, Esma anaujua mchezo mzima na anatajwa kuusambaza ubuyu huo kama
malipo kwa Wema (Sepetu) anayemtuhumu kumuibia bwana wake, Petit Man.
“Esma
ameamua kumwaga ugali maana Wema na timu yake wamekuwa wakijitapa sana
mjini kwamba wamemnyakua mume wa Esma, Petit Man. Na yeye anawaonesha
kwamba kama ni kuchukuliwa mbona hata Kajala amechukuliwa na Diamond
ambaye alikuwa mtu wa Wema lakini wamekaa kimya,” alisema msanii huyo.
Jitihada
za kumpata Esma ili aweze kuzungumzia suala hilo ziligonga mwamba baada
ya simu yake ya mkononi kuita muda mrefu bila kupokelewa.
MITANDAO YAZIDI KUKUZA JAMBO
Mpaka
tunakwenda mitamboni, juzi, mitandao mbalimbali hususan Instagram,
wadau walisambaza habari ya Kajala na Diamond huku wakijaribu kumwambia
Zari amtambue Kajala kama mke mwenzie kwani ameshalala Madale, nyumbani
kwa Diamond.
“Zari mke mwenzio ni huyu hapa, anakusaidia. Juzi amelala Madale na Diamond,” iliandikwa na mdau mmoja wa Instangram.
ZARI ACHANGANYIKIWA
Chanzo
kilichomwaga ubuyu huo kimeeleza kuwa, taarifa za Kajala na Diamond
zilipomfikia Zari, alichanganyikiwa na kuanza kumcharukia Diamond au
baba Tiffah ambaye ilibidi atumie nguvu ya ziada kumtuliza kwani bado
wawili hao wanaendeleza uhusiano wao huku wakijua Zari hayupo Bongo.
“Zari
alicharuka kwelikweli. Ilibidi Diamond atumie nguvu ya ziada kumtuliza
na bahati nzuri mtoto wa kike ameelewa,” kilisema chanzo chetu.
DIAMOND SASA
Alipotafutwa Diamond na kusomewa mashitaka yake, mambo yalikuwa hivi:
Risasi Jumamosi:
Kuna taarifa kwamba unatembea na Kajala na sasa mahaba ni motomoto,
vipi kuna ukweli? Tena vyanzo vingine vinadai kuna hadi picha za wewe na
Kajala mkiwa nyumbani kwako, unazungumziaje hilo?
Diamond: Aaah! Siyo kweli mwanangu...picha kweli mnazo? Picha gani...yaani kiaje?
Risasi Jumamosi: Inasemekana zipo ambazo mpo nyumbani kwako, Madale.
Diamond: Aahaha! Aaah uongo mtupu siyo kweli. Kama kuna picha kweli nitumieni basi.
KAJALA SASA
Alipopigiwa simu zaidi ya mara tano, Kajala hakupokea. Risasi Jumamosi lilimtumia ujumbe mfupi wa maneno (SMS) uliosomeka hivi:
“Habari,
kuna ishu yako hapa Global Publishers, inahusu madai ya wewe kutoka
kimapenzi na Diamond jambo ambalo linadaiwa kuleta mtafaruku mkubwa kati
yako na Zari. Pia hata kwenye mitandao ya kijamii bila shaka umesikia,
naomba ufafanuzi wako tafadhari.”
Licha ya ujumbe huo kuonesha kumfikia, hadi tunakwenda mitamboni, Kajala hakujibu chochote.
KAMA NI HIVYO
Madai
ya kuwepo kwa uhusiano huo yanaweza kumweka Kajala katika mtazamo
mwingine kijamii, kwani miaka miwili nyuma alidaiwa kutoka kimapenzi na
mwanaume anayeitwa CK ambaye hakuna shaka alikuwa mpenzi wa Wema kabla
ya kumwagana.
Hali
hiyo ilizua mjadala, Kajala alibebeshwa madai mazito kwamba alikuwa na
uhusiano na CK hata akiwa na Wema, ikitafsiriwa kwamba alikuwa akimlia
vyake mwenzake hali iliyozua mgogoro wa wawili hao.
Diamond
naye, amewahi kuwa na uhusiano wa kimapenzi na Wema, wakamwagana.
Kitendo cha kudaiwa kutoka na Kajala, kinazidi kumweka mdada huyo katika
mlolongo wa kudhaniwa anamwandama Wema kwa vile kila alikopita, yeye
naye anapita!
CHANZO: GAZETI LA RISASI JUMAMOSI
Post a Comment