Magufuli Atikisa Mitandao Ya Kijamii Nchi Kenya.......Wakenya Wammwagia Sifa Kibao, Watamani Awe Rais Wao

 

Uchapakazi wa Rais Dkt John Magufuli unatuma ujumbe si kwa maafisa wa Tanzania pekee, bali na nchi za jirani pia na kuwaacha viongozi wa nchi hizo kwenye wakati mgumu.
 
Kenya ambayo imekuwa ikifuatilia siasa za Tanzania tangu wakati wa kampeni, imeonesha kupenda mbinu za Magufuli na wananchi wake wanatamani mtu kama yeye.
 
Kwa kipindi kifupi alichoingia madarakani, Magufuli amefanya mambo makubwa na wananchi wamependa.
 
Ziara yake ya kushtukiza kwenye hospitali ya Muhimbili ilifichua uovu mwingi na kupelekea kufutwa kwa bodi ya wakurugenzi wa hospitali hiyo na kumuondoa Kaimu Mkurugenzi wake, Dk Hussein Kidanto.
 
Ili kupunguza matumizi makubwa ya fedha za serikali kwaajili ya kugharamia safari za nje za viongozi wa nchi, Magufuli aliamua kuzisitisha mara moja.
 
Dkt Magufuli pia alielekeza kiasi cha shilingi milioni 225 zilichangwa kwaajili ya kugharamia hafla ya wabunge kupongezana mjini Dodoma zipelekwe kwenda kununua vitanda. Badala yake shilingi milioni 15 pekee zilitumika kwaajili ya sherehe hiyo. 
 
Siku chache baadaye vitanda hivyo na vifaa vingine vilinunuliwa na kupelekwa Muhimbili.
 
Jumatatu hii Magufuli alitangaza kuondoa sherehe za maadhimisho ya siku ya Uhuru December 9 na fedha za maandalizi hayo zitumike kwa mambo mengine muhimu.
 
Hayo na mambo mengine yamefanya Dkt Magufuli atrend nchini Kenya.
 
Hizi ni baadhi ya tweets za wakenya:



Post a Comment

Previous Post Next Post