Rose Ndauka: Naapa sitazaa tena nje ya ndoa!




Mwanadada anayeuza nyago kwenye filamu Bongo, Rose Ndauka.

MWANADADA anayeuza nyago kwenye filamu Bongo, Rose Ndauka ameapa kuwa sasa hivi atajitahidi sana kuhakikisha hazai tena nje ya ndoa kwani anajua amemkosea Mungu na ndugu zake pia.
Akipiga stori  Rose alisema anajua alifanya kosa kujiachia na kubeba mimba nje ya ndoa lakini sasa amejifunza na hawezi kurudia kosa hilo.
“Sasa hivi niko makini kuliko mnavyofikiria, najizuia sana kuhakikisha sizai tena kabla ya kuingia kwenye ndoa. Yaani nitakuwa ni mwenye amani endapo mtoto wangu wa pili nitamzaa nikiwa ni mke wa mtu, Mungu anisaidie katika hilo,” alisema Rose.

Post a Comment

Previous Post Next Post