Mmoja wa wachezaji wanaowania tuzo za Caf mwaka huu, Andrew Ayew..
Shirikisho la Soka barani Africa limeyataja majina 10 ya wachezaji wanaowania tuzo ya mchezaji bora barani Afrika kwa mwaka wa 2015. Katika majina hayo pia ameorodheshwa mchezaji bora kwa mwaka 2014, Mchezaji wa timu ya taifa ya Ivory Coast na klabu ya Mnachester City.
Kwa upande wa taifa nchi ya Algeria na Ivory Coast yamefanikiwa kuingiza wachezaji wawili kila moja kwa upande wa Algeria wachezaji ambao wameingia katika orodha hiyo ni  Sofiane Feghouli anayekipiga katika klabu ya Valencia inayoshiriki Ligi kuu ya nchini Hispania (Primera Division) na mchezaji mwingine ni Yacine Brahimi anayekipigiga katika klabu ya Porto inayoshiriki Ligi kuu ya Ureno.
Kwa taifa la Ivory Coast imemuingiza Serge Aurier anayekipiga katika klabu ya Paris Saint-German inayoshiriki ligi kuu ya Ufaransa (Seria A) na Yaya Toure anayechezea Manchester City inayoshiriki ligi ya Wingereza (Primear League)
Wachezaji hao ni pamoja na Andre Ayew (Ghana-Swansea City), Aymen Abdennour   ( Tunisia-Valencia), Mudather Eltaib Ibrahim (Sudan-Al-Hilal), Mohamed Salah (Egypt-Roma), Pierre-Emerick Aubameyang (Gabon-Dortmund), Sadio Mane (Senegal-Southampton), Serge Aurier (  Ivory Coast-Paris Saint-German), Sofiane Feghouli (Algeria-Valencia).
Pia wapi Yacine Brahimi (Algeria-Porto) na Yaya Toure ambaye anashikilia tuzo hiyo aliyoitwaa mara mbili mfululizo katika misimu miwili iliyopita akitokea  Ivory Coast na klabu ya Manchester City.