Burudani za Krismasi Diamond ndani ya Dar Live 
GOOD news ikifukie kwako mpenda burudani kwamba baada ya kusumbua na Ngoma ya Nana ‘Sankoro’, King wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ jana (Ijumaa) kupitia mitandao, redio za ndani na nje ya nchi ameshusha ngoma yake mpya.

Ikumbukwe kuwa hadi sasa ngoma ya Nana iliyotoka rasmi Mei mwaka huu ni moja ya ngoma kali za Diamond zilizofanya vizuri na kumuongezea wigo wa soko la muziki ndani na nje ya nchi.
Tuzo
Moja ya mafanikio aliyoyapata Diamond mwaka huu kupitia Ngoma ya Nana ambayo kideo chake kimefanywa na Kampuni ya Godfather nchini Afrika Kusini ni kuibuka na tuzo kibao kama vile MTV Europe (EMA), African Muzik Magazine (Afrimma), Nollywood & African Films Critics (Nafca) na nyingine kibao.
Rekodi
Kwa takriban mwaka mmoja, Ngoma ya Nana imeweka rekodi katika mtandao wa Youtube kuwa miongoni mwa ngoma za Diamond zilizotazamwa na mashabiki wake mara nyingi zaidi ikiwa ni mara milioni 7,268,108.
Ngoma zake nyingine zilizotazamwa mara nyingi ni Mdogomdogo iliyotoka mwaka jana ambayo imetazamwa mara 5,086,813. Nayo Ntampata Wapi iliyotoka Desemba mwaka jana imetazamwa mara 6,597,653 pamoja na Nasema Nawe iliyotoka Aprili mwaka huu ambayo imetazamwa mara 5,531,289.
diamond-23.jpgNgoma mpya je?
Mashabiki wengi wa Diamond na Muziki wa Bongo Fleva wanatarajia kuona ngoma ya leo ikiweka rekodi ya aina yake kwa kusikilizwa na kutazamwa mara nyingi zaidi ndani na nje ya nchi sambamba na kumletea mafanikio kama ilivyokuwa kwa Nana.
Akizungumzia ngoma mpya, Diamond alisema kwanza itakuwa ni moja ya ngoma zake kali zote alizowahi kuzitoa. “Kama ilivyo kawaida yangu sina maneno mengi, ngoma itajieleza yenyewe na hii ni sapraizi kubwa kwa mashabiki wangu,” alisema Diamond.
Kuitambulisha Dar Live
Kwa mara ya kwanza baada ya kuachiwa ngoma hiyo mpya, Diamond ataizindua rasmi Sikukuu ya Krismasi (Desemba 25) mwaka huu ndani ya Uwanja wa Taifa wa Burudani, Dar Live uliopo Mbagala- Zakhem jijini Dar.
Ikumbukwe kuwa mara ya mwisho kwa Diamond kufunika Dar Live ilikuwa Krismasi mwaka jana katika bonge moja la shoo lililokuwa likitambulika kama Usiku wa Wafalme akiwa na Mfalme Mzee Yusuf ambapo Diamond alikamua ngoma zake zote kali kama vile Ntampata Wapi, Mdogomdogo na nyinginezo.
IMG_9148Msaga Sumu kusindikiza
Katika kunogesha Sikukuu ya Krismasi Dar Live, mbali na Diamond kukamua na madensa wake, bingwa wa muziki wa Singeli, Msagasumu naye atakuwepo jukwaani kukamua ngoma zake zote kali.
Siku hiyo Msagasumu ataimba ngoma yake iitwayo Inaniuma Sana aliyomshirikisha Nature, Huyo Mtoto, Shemeji Unanitega, Naipenda Simba na nyingine kibao.
002.NUSU FAINALIWakali Dancers nao ndani
Mabingwa wa sarakasi, kucheza muziki wa kila aina, Wakali Dancers nao watakuwepo kukamilisha hamu ya mashabiki wa burudani.

No comments:

Post a Comment