EXLUSIVE!! Nicki Minaj kuolewa mwakani



 Rapa Meek Mill, akiwa na mpenzi wake diva wa Hip Hop, Nick Minaj.

EXLUSIVE!! BAADA ya kuvishwa pete kwa mara nyingine na rapa Meek Mill, diva wa Hip Hop, Nick Minaj yupo mbioni kuolewa ambapo inasemekana mwakani (2016) ndiyo ataolewa.

Chanzo kilipenyeza ‘ubuyu’ kuwa Nicki anafanya kila awezalo kuhakikisha jamii kwa ujumla inaelewa haraka kwa vitendo kuwa ndoa yake imekaribia.

nicki-minaj-ring“Nicki amempa Meek nafasi kubwa ya kukubali kuvaa pete kwa ajili yake, anataka kutengeneza maswali kwa mashabiki na kweli amedhamiria kuvishwa rasmi pete ya ndoa na kuolewa mwaka 2016,” kilisema chanzo.

Jana kupitia ukurasa wake wa Instagram, Nicki aliweka picha ya mkono ikiwa na pete ya uchumba.

Post a Comment

Previous Post Next Post