Johari: Chipukizi msitoe penzi

STAA wa filamu Bongo, Blandina Chagula ‘Johari’ amewasihi wasanii chipukizi wa kike kuacha kutoa penzi kwa mastaa wakiamini watawasaidia kutoka kisanaa, kwani haitawasaidia.

Akipiga stori na paparazi wetu hivi karibuni, Johari alisema wasanii wengi wanapata vishawishi vya kutakiwa kutoka kimapenzi kwa ahadi ya kusaidiwa, kitu ambacho siyo kweli kwani kitu pekee kitakachoweza kuwasaidia kuibuka ni juhudi zao za kazi.

“Wengi wao hawajitambui, wanafikiria labda wakitembea na staa f’lani basi ndiyo watatoka haraka, nawasihi wapiganie malengo yao kwa kupiga kazi na siyo kwa kutumia miili yao, mimi mwenyewe napiga kazi kwa nguvu zangu mwenyewe,” alisema.

No comments:

Post a Comment