Watu zaidi ya 15 wamedaiwa kukivamia kituo cha redio cha Hits FM cha visiwani Zanzibar na kukiteketeza kwa moto.
Studio ya Hits FM baada ya kuchomwa moto
Watu hao wanadaiwa walikuwa kwenye gari aina ya Noah waliyoipaki nje ya ofisi hizi, kuwashambuliwa walinzi na kuwazidi nguvu kabla ya kuingia kwenye studio za redio.
Tukio hilo limetoa usiku wa kuamkia Alhamis hii, saa saba na dakika 40.
Mtangazaji
wa kituo hicho, Sophy Dalah ameiambia Bongo5 kuwa watu hao walipoingia
walimshikilia mtangazaji wa zamu na kumwekea matambala mdomoni kumzuia
asipige kelele.
“Watu hao walikuwa wamejifunika sura zao kama Ninja, walimwambia ‘uko chini ya ulinzi kwa wakati huu tunaomba ushuke kwenye kiti cha utangazaji na tunachokuambia tunaomba ufuate,” amesema mtangazaji huyo wa kipindi cha Power Artist kinachoruka kwenye kituo hicho.
“Wakamfunga
uso, wakamfunika ili asijue nini kinachoendelea wakamwekea matambala
mdomoni hatimaye wakamtoa nje. Walimpiga piga mapanga lakini sio kwa
kumuumiza, bali walikuwa wakimtishia tu,” ameongeza.
Amesema watu hao wamechoma studio ya kurushia matangazo na ya kufanyia utayarishaji wa vipindi.
Hata hivyo amesema bado hawajajua sababu ya watu hao kukivamia kituo hicho na kwamba polisi wanaendelea na uchunguzi.
Ameongeza kuwa uongozi wa kampuni hiyo umewapa likizo ya kipindi kisichojulikana

إرسال تعليق