Mwanamke msagaji amlainisha Kidoa kwa gari na Nyumba




 Video Queen anayekuja juu kwa kasi ya ajabu, Asha Salum ‘Kidoa’.
Video Queen anayekuja juu kwa kasi ya ajabu, Asha Salum ‘Kidoa’ amejikuta kwenye wakati mgumu kufuatia mwanamke mmoja msagaji wa jijini Dar kumtokea na kumtaka ampe penzi.

Akizungumza  huku akionekana kuwa na hasira, Kidoa alisema kuwa anamshangaa mwanamke huyo kumtumia meseji kila wakati akidai kuwa akimkubalia atahakikisha anaishi kwenye nyumba nzuri na kumpa gari la kutembelea.

“Huu ustaa unanitokea puani, kuna mwanamke mmoja ambaye anaonekana kabisa ni msagaji amekuwa akinitumia sms na kuniambia eti kaniona kwenye magazeti na mitandao na kavutiwa na mimi.

“Najiuliza kavutiwa na mimi kivipi wakati ni mwanamke mwenzake? Jibu nikapata kuwa atakuwa ni msagaji, nimemtukana sana kwani sijapenda.

“Yaani anahisi mimi nina tabia hiyo chafu, alidhani mimi ni kama wale, ningemjua ningemshtaki,” alisema Kidoa huku akionesha sms chafu ambazo mwanamke huyo amekuwa akimtumia.

Mwandishi wetu alifanya jitihada za kumpigia simu mwanamke huyo lakini iliita bila kupokelewa, alipotumiwa sms pia hakujibu. Namba yake ameisajili kwa jina la Gift John. Jitihada za kumjua ni nani na ana nia gani na Kidoa zinaendelea.

Post a Comment

Previous Post Next Post