Rayuu afungukia ishu ya mastaa wengi kupenda kwenda kujiuza nchi za nje



MSANII wa filamu Bongo, Alice Bagenzi ‘Rayuu’ amefungukia ishu ya mastaa wengi kupenda kwenda kujiuza nchi za nje ikiwemo Sauzi akisema kuwa, wanaofanya hivyo hawajitambui na kinachowasumbua ni tamaa ya pesa.

Akipiga stori na paparazi wetu hivi karibuni, Rayuu alisema alishasumbuliwa na wadada wengi wakimpa madili ya kwenda kujiuza China, Sauzi na kwingineko lakini akawatolea nje kutokana na msimamo alionao

“Unajua hakuna kinachowapeleka huko zaidi ya tamaa kwa kuwa kule wanalipwa kwa dola wakirudi huku wakizibadilisha wanapata pesa nyingi, halafu huku unakuta mtu ameshatembea na wanaume wengi ndiyo maana anakimbilia nje,” alisema Rayuu

Post a Comment

Previous Post Next Post