Wastara Juma afunguka kitu ambacho kimemponza!STAA wa filamu Bongo, Wastara Juma amesema kitu ambacho kimemponza na kumfanya asumbuliwe na mguu wake mara kwa mara ni kujisahau sana katika starehe kwa kuwa hajawahi kujikubali kuwa ni mlemavu.

Akipiga stori na paparazi wetu Wastara alisema, tangu alipopatwa na tatizo hilo la mguu kwenye fikra zake hakutaka kukubali matokeo, siku zote alipenda aishi kama alivyokuwa mzima ikiwa ni pamoja na kwenda kwenye muziki na kucheza.

“Siyo siri nilijisahau sana, sikupenda kujiona mlemavu, nilikuwa naishi kama mtu wa kawaida tu.

Sasa hivi najuta kwa kutozingatia matunzo ya mguu wangu maana nilikuwa najiachia sana hususan linapokuja suala la muziki. Sasa nimeamua kukubaliana na hali halisi kama walivyo walemavu wengine,” alisema Wastara.

CHANZO: GPL

No comments:

Post a Comment