Waimbaji wa yamoto bendi wakiwa katika picha ya pamoja.
Na Mwandishi Mwetu
WAKATI
jana wakiendelea kutoa burudani katika mji wa Washington DC, Bendi ya
Yamoto, imeingia katika kuwania tuzo za Kora 2016, ikiingia katika
kipengele cha Most Promising Male Artist Of Africa.
Mkurugenzi
wa bendi hiyo Said Fella, alisema kwanza anamshukuru Mungu vijana wake
juzi usiku walikuwa na onesho lao la pili lililofanyika Washington DC na
kuweza kufanya vizuri, lakini la pili kuingia katik tuzo za Kora.
Fella ambaye ni diwani wa Kata ya Kilungule alisema ni kitu kikubwa sana kwake kwa bendi yake kuingia katika tuzo za Kimataifa.
Alisema
kuingiaa kwa vijana wake katika tuzo hizo ni kitu kikubwa sana na
kinazidi kuipandisha bendi yake ambayo sasa ipo nchini Marekani kwa
ziara ya maonesho maalum.
"Ni
kitu kikubwa sana kinazidi kutupandisha kutoka sehemu moja kwenda
kwingine, tunaamini mwenyezi Mungu atatusimamia tuweze kupata kwa
mashabiki wetu kuliona hili na kutuunga mkono katika kupiga kura"alisema
Fella.
Kwa
upande wa ziara ya bendi yake nchini Marekani alisema vijana hao
watafanya onesho la mwisho Desemba 12, katika mji wa Houston na baadae
kurejea nchini kwa kazi zao nyingine.
Alisema
katika onesho la juzi walifanya onesho zuri la aina yake na katika mji
wa Washington na kuudhuliwa na mashabiki wengi wa muziki.
"Onesho letu la juzi lilikuwa zuri sana na limezidi kuongeza
hamasa kwa vijana wazidi kujituma na kufanya viuri zaidi katika
kuhakikisha wanapata mihaliko kama hii ya kuja nchini kama hizi ambazo
nazo tumekuwa na mashabiki wetu"alisema Fella

إرسال تعليق