Sababu ya Wasanii kukataa kulipwa na kuikataa COSOTA



Kupitia #PLANETBONGO @nikkwapili ametoa ufafanuzi kuhusu wasanii kutoa mapendekezo kusitisha mpango wa kulipwa mirabaha na mapendekezo ya kuvunjwa kwa bodi na management ya chama cha hatimiliki Tanzania #COSOTA .HAYA NDIYO ALIYOSEMA… -Kwanza taasisi iliyopewa tenda hiyo #CMEA inamilikiwa na kampuni ya #PUSHMOBILE ambayo wasanii wameshuhudia kua INA historia mbaya ya kuwaibia wasanii kwahyo hawawez kuwaamini tena. -Pili Sheria iliyounda #COSOTA inasema lazima iundwe na kusimamiwa na wasanii wenyewe lkn haipo hivyo.kwahyo wasanii wanataka #SHERIA ichukue mkondo wake na #cosota isimamiwe na iongozwe na wasanii.
Pia bodi ya COSOTA haiundwi na wasanii na pia #UTENDAJI wa COSOTA siyo wa kurizisha ikiwemo kuwashauri wasanii issue za kimuziki ni jukumu lao lkn hawafanyi hivyo. -Kingine ni mazingira ya ulipaji mirabaha YANAONEKANA HAYAPO TAYARI.mfano wanasema Mziki utakaopigwa uwe wa nje au ndani (_ya nchi)utalipiwa,wakati huo huo wanasema ili wimbo ulipiwe lazima usajiliwe COSOTA na #CMEA ,lkn ukwel in kua nyimbo nyingi za nje na za nyumban hazijasajiliwa Popote kati ya taasisi hizo. -Kadhalika wanasema #MAUDHUI ya #Media za nyumbani 60% nyumbani na 40% ya nje na sheria hii imekuwepo kwa miaka mingi lakini ukiangalia uhalisia hasa kwa vituo vya #Tv hapa Bongo maudhui yake 80% ni ya nje.
Kwamaana hiyo usimamizi huo haupo na wasanii hawawezi kusaini na kukubalina na mambo yasiyokuwepo kiuhalisia. -mwisho Ukiangalia hii sheria wanasema ni makubaliano ya kiukanda wa #AfricaMashariki kuwa media zipige 60% local content lakini ukiangalia #kenya mambo ya mirabaha yalipoanza media zilianza kupiga 80% maudhui ya nje na kwahyo hii sheria haina #Uhalisia

Post a Comment

Previous Post Next Post