Imebainika kuwa Tanzania inakabiliwa na changamoto ya kuwaajiri mahotelia wasio kuwa na ujuzi wa kutosha  katika sekta ya utalii haswa kwenye hoteli hali ambayo inarudisha  nyuma uchumi wa  nchi tofauti na nchi nyinginezo  za nje ya nchi.
Hayo yalisemwa na Meneja mkazi wa kampuni ya Jovago Tanzania, Andrea Guzzoni alipokuwa akizungumza na vyombo vya habari katika uzinduzi  wa ripoti ya mwisho yenye utafiti inayohusiana na sekta ya utalii ili kuweka wazi hali inayoikabili sekta hiyo.
Alisema kuwa sekta ya utalii kwa hapa Tanzania imekuwa ikipanda na kushuka mwaka hadi mwaka lakini  bado ina changamoto ya kuwaajiri wafanyakazi kwa mazoea badala ya kuwaajiri wenye ujuzi wa kutosha hali ambayo amesema kuwa inapaswa kuangaliwa kwa upya ili kuiwezesha sekta hiyo kupanda kiuchumi.
Aliongeza kuwa ili Tanzania iweze kufikia watalii milioni mbili  miaka ijayo  serikali inapaswa kuangalia utaratibu wa kuwachukua mahotelia na kuwapeleka nje ya nchi ili waweze kujifunza jinsi ya kuhudumia wageni  kwani wapo wengine ambao hawajui lugha na hata jinsi ya kuhudumia wageni wanaongia nchini  hali inayowafanya  watalii kukosa huduma nzuri.
Aidha Guzzoni aliwataka wadau wote ndani ya sekta ya utalii kuhakikisha wananchangamkia fursa ya kujitangaza na kuonyesha utofauti wao kwa umahiri ili kusaidia watanzania wenye nia na maendeleo na utalii wa ndani.
Kwa upande wake Afisa Habari na Uhusiano wa kampuni hiyo, Lilian Kisasa akizungumza katika uzinduzi huo alisema kuwa kwa hapa Tanzania sekta ya utalii imeweza kuajiri watu zaidi ya laki sita na endapo huduma nzuri zitaboreshwa katika sekta hiyo upo uwezekano wa kuajiri watu zaidi ya hapo jambo ambayo itapunguza hata tatizo la ajira hapa nchini.
unnamed (3)
Afisa habari na uhusiano wa kampuni  Jovago Tanzania  Lilian Kisasa na Meneja mkazi wa kampuni ya Jovago Tanzania Andrea Guzzoni katika uzinduzi huo.
unnamed (2)
Meneja mkazi wa kampuni ya Jovago Tanzania, Andrea Guzzoni alipokuwa akizungumza na vyombo vya habari katika uzinduzi  wa ripoti ya mwisho yenye utafiti inayohusiana na sekta ya utalii ili kuweka wazi hali inayoikabili sekta hiyo.
unnamed
Afisa habari na uhusiano wa kampuni Jovago Tanzania, Lilian Kisasa akizungumza katika uzinduzi huo ambapo alisema hapa Tanzania sekta ya utalii imeweza kuajiri watu zaidi ya laki sita na endapo
huduma nzuri zitaboreshwa katika sekta hiyo upo uwezekano wa kuajiri watu zaidi ya hapo jambo ambalo litapunguza hata tatizo la ajira hapa nchini.(Pamela Mollel jamiiblog)
unnamed (1)
Wanahabari wakiwa katika uzinduzi wa ripoti.