Wasanii
wa muziki mbalimbali hapa nchini, Jumamosi hii wanatarajiwa kukinukisha
vilivyo katika Viwanja vya Mwembe Yanga Temeke jijini Dar es Salaam,
katika tamasha la Amsha Mama Festival.
Akizungumza
kwa niaba ya wasanii wenzake, Balozi wa tamasha hilo Khalid Ramadhani
‘Tundaman’, ambaye amepewa Ubalozi huo kupitia waandaaji wa tamasha la
(AFWAB) AMSHA MAMA Festival 2016, lililo chini ya Mkurugenzi Mtendaji
wa lebo ya Candy na Candy Records Joe Kariuki, alisema tamasha hilo
linalotarajiwa kufanyika Machi 5 mwaka huu katika uwanja wa Mwembe Yanga
jijini Dar es Salaam.
Tundaman
na Muandaaji wa tamasha hilo Kariuki, wamesema kwamba maandalizi ya
shoo hiyo tayari yameshakamilika kwa kiasi kikubwa hivyo angependa
kutumia fursa hii kuwaalika wakazi wote wa jiji la Dar, kujumuika siku
hiyo kushuhudia burudani mbalimbali zitakazotolewa na wasanii kibao
ambao tayari wemedhibitisha kufanya makamuzi siku hiyo.
“Tunapenda
kuwaalika Watanzania wote kwa ujumla siku ya jumamosi hii ya Machi 5,
mwaka huu waje kwa wingi katika Viwanja vya Mwembe Yanga Temeke jijini
Dar Salaam, ili tujumuike kwa pamoja katika tamasha la kuhamasisha
wanawake kujikwamua katika shughuli zao mbalimbali za kiuchumi.
Tamasha
hili litakuwa ni la wazi kwa maana kwamba watu wote watapata burudani
kibao bila malipo yaani bure kabisa hivyo waje kuwashuhudia wasanii
kama, Khadija Kopa, Mr Blue, Snura, Msaga Sumu, Ali Chocky na Tunda Man
wakitoa burudani ya hali ya juu kwani ulinzi na usalama siku hiyo ni wa
uhakika,” alisema Tunda Man.
Kwa
upande wake, Joe Kariuki ambaye ni mratibu mkuu wa tamasha hilo
ametumia muda huu kuongea na baadhi ya akinamama wanaojishughulisha na
biashara za vitu mbalimbali hususani mama ntilie, wauza matunda na
wauzaji wa mitumba ili nao wajitokeze kwa wingi kuja kunadi bidhaa zao
siku hiyo kwani hiyo ndiyo fursa yao ya kipekee ya kujitangaza bure.
Msanii Tundaman.
Post a Comment