Yanga vs TP Mazembe June 28 2016, kiingilio ni bure

Jumamosi ya June 25 2016 mkuu wa idara ya habari na mawasiliano wa klabu ya Dar es Salaam Young Africans Jerry Muro alitangaza viingilio vya mechi yao ya Kombe la Shirikisho barani Afrika dhidi ya TP Mazembe itakuwa na kiingilio kati ya Tsh 7000 hadi 30000.
Taarifa zilizotoka June 26 kuelekea mchezo huo wa pili wa Kundi A lenye timu za MO Bejaia ya Algeria, TP Mazembe, Medeama ya Ghana na Yanga, uongozi wa klabu ya Yanga wametangaza kuwa mechi yao wameamua mashabiki waingie bure ili waweze kuishangilia timu yao.
yng
Maamuzi hayo ya Yanga,  wadau na mashabiki wa soka wanatafsiri kama ni maamuzi ya hasira na yanatajwa kuja kutokana na TFF imewakosea kuingia mkataba na Azam TV wa kurusha mechi hiyo live pasipo wao kushirikishwa, wakati wao wanaamini kuwa mechi hiyo ikioneshwa Dar es Salaam watakosa mapato.

No comments:

Post a Comment